Shule ya Lucky Vincent |
SERIKALI
ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania itagharamia shughuli za mazishi ya
wanafunzi 33, walimu wawili na dereva mmoja waliopoteza maisha kwenye
ajali ya basi iliyotokea kwenye kata ya Rothia baada ya kutumbukia
kwenye korongo la mto Malera.
Kwa mujibu wa Meya wa jiji la Arusha, Mhe. Calist Lazaro amesema gharama hizo ni pamoja na kununua sanda pamoja na majeneza.
Meya wa Arusha, Calis Lazaro |
Akitoa
taarifa hiyo leo Mei 7, 2017, Meya huyo alisema kuwa taarifa za awali
zinaonyesha kuwa tayari Serikali imekwishalipia gharama za majeneza na
sanda ya kuhifadhia miili ya marehemu ambapo kesho kwenye uwanja wa
kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, patafanyika ibada ya kuaga miili ya
mareghemu.
SHULE YAFUNGWA
Shule
ya Lucky Vicent imefungwa kwa siku saba kufuatia vifo vya wanafunzi
wake 33, Walimu wawili na dereva mmoja vilivyotokea kwenye ajali ya gari
Juma wilayani Karatu, mkoani Arusha.
Mbunge wa Arusha, Mhe.Godbles Lema |
Kutokana na ajali hiyo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na wabunge wengine wa Chadema wamefika shuleni hapo kutoa pole.
Lema
kwa niaba ya wabunge wenzake ameeleza kusikitishwa na msiba huu na
amewapa pole wafiwa lakini akatoa angalizo kusiingizwe siasa katika
msiba huu mkubwa.
Meya
wa jiji la Arusha Mstahiki Calist Lazaro ameeleza kuwa Waziri wa Afya,
Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene na Waziri wa
Elimu, Profesa Joyce Ndalichakowalitarajiwa uwasili jioni hii ya Jumapili Mei 7, 2017 ili kuzungumza na jumuiya ya wshule ikiwa ni pamoja na wafiwa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
ataongoza watanzania kwenye ibada ya kuaga miili ya marehemu hao kwenye
uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuanzia saa 3
asubuhi, hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.
Mrisho Gambo.
Mkuu
wa shule hiyo, Ephraem Jackson amesema hadi sasa vifo ni 36 na
wanafunzi wawili bado wamelazwa Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.
Wanafunzi hao ni Sadiely Ismail na Wilson Tarimo.
0 comments:
Post a Comment