Frank
Mvungi-Maelezo
Kuelekea
Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara Serikali imepongezwa kwa Mafanikio
yaliyofikiwa katika kipindi chote tangu awamu ya kwanza hadi awamu ya tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo wakati wa mahojiano
maalum kuhusu maadhimisho ya miaka hamsini na tano ya Uhuru yanayotarajiwa kufanyika kitaifa tarehe 9 Desemba mwaka huu.
“Tumepiga
hatua kubwa katika upatikanaji wa huduma za jamii kama vile elimu,Afya,Maji,usafirishaji
na miundo mbinu ukilinganisha na wakati tunapata Uhuru” Alisisitiza Chongolo
Katika Sekta
ya elimu Chongolo anabainisha kuwa Serikali katika awamu zote tangu awamu ya
kwanza hadi sasa zimekuwa zikiweka kipamaumbele katika Sekta hiyo hali iliyochangia kuongezeka kwa shule
za msingi ,Sekondari na Vyuo Vikuu .
Akifafanua zaidi
Chongolo ameongeza kuwa elimu bure ni miongoni mwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya tano ya kuwaletea wananchi wake maendeleo na kuzidi
kuendeleza azma ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya
kupamabana na maudui watatu ambao ni ujinga,maradhi na umasikini.
Akizungumzia
kuhusu miundo mbinu ya barabara anabainisha Tanzania ya sasa ina tofauti kubwa
na wakati Taifa lilipokuwa likipata Uhuru ambapo barabara za lami na madaraja
yalikuwa machache lakini hivi sasa Mikoa yote inafikika kwa urahisi.
Anaongeza
kuwa sekta ya maji pia imeimarika ukilinganisha na wakati wa uhuru ambapo moja
ya miradi mikubwa iliyotekelezwa na Serikali ni mradi wa maji wa ziwa Victoria
hadi shinyanga na mwingine ni ule wa upanuzi wa mitambo ya Ruvu juu na Ruvu
Chini ambayo imeanza kumaliza tatizo la maji katika Jiji la Dar es salaam.
Aidha
Chongolo aliwaaasa wananchi kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa rasilimali za
Taifa na miundo mbinu iliyopo kwa maslahi ya taifa kwa kuwafichua wale wote
wanaokwaamisha au kuhujumu nia njema ya Serikali katika kuwaletea wananchi
maendeleo.
Sherehe za
Uhuru huadhimishwa kila mwaka inapofika tarehe 9 mwezi Desemba ambapo mwaka huu
Kitaifa zitafanyika Jijini Dar es salaam na Kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe mwaka mmpja uliopita.
Kauli mbiu
ya maadhimisho hayo ni “Tuunge Mkono
Jitihada za Kupinga Rushwa,Ufisadi na Kuimarisha Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo yetu.”
MWISHO
0 comments:
Post a Comment