Arusha
Home » » MOBISOL NA ZUKU TV WAZINDUA HUDUMA ZA TELEVISHENI YA SATELITE YA NISHATI YA JUA

MOBISOL NA ZUKU TV WAZINDUA HUDUMA ZA TELEVISHENI YA SATELITE YA NISHATI YA JUA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 Meneja Mkuu wa Zuku Tv Tanzania  , Bw.Omari Zuberi akiongea na waandishi wa habari juu ya huduma mpya ya TV ya nishati ya jua ambayo ina channel za Zuku Tv
 katikati ni Afisa masoko wa Mobisol Sjors Martens akiwa na wafanyakazi wa mobiso l katika uzinduzi huo hii leo jijini Arusha
 mmoja wa mmteja wa mobisol ambaye akutaka kutaja jina lake akiongea wakati wa uzinduzia ambapo aliisifia kampuni ya mobisol nakusema ni mtetezi wa wananchi wanaoishi vijijini ambapo umeme haujafika
 Meneja wa zuku Tanzania wa kwanza kushoto akibadilishana mawazo na wa kwanza kulia ni afisa usiano wa Zuku  dada Yasta pamoja na  mwakilishi wa zuku  Jack Karanja katika uzinduzi
 wafanyakazi wa zuku wakifurahia mara baada ya uzinduzi



            
 Na Woinde Shizza,Arusha

 KAMPUNI inayoongoza kwa utowaji wa huduma za nishati ya jua majumbani ,Mobisol na Kampuni ya Zuku Tv inayotoa burudani za satellite wameungana  pamoja kwa ajili kuwanufaisha watanzania wasiounganishwa na nishati ya umeme. 

Kwa pamoja kampuni hizi zimezindua kwa mara ya kwanza TV ya nishati ya jua ambayo ina channel za Zuku Tv  huduma inayowalenga wale ambao hawajafikiwa na umeme wa gridi ya Taifa.



Huduma hii huunganisha mfumo  wa nishati jua, televisheni ya hadi inchi 32 ya nishati jua, ungo wa satellite, na huduma ya ya kifurushi cha Zuku Smart Plus chenye chanelli 47 and 18 za redio. Mobisol wanalenga  kutoa huduma hii kwa watanzania ambao hawajafikiwa na huduma ya nishati ya umeme, kwa  kutoa nashati safi na ya kuaminika kwa bei nafuu popote ulipo katika mfumo moja mkamilifu.



Mobisol inatoa vifurushi mbalimbali vya nishati ya jua ya majumbani, vilivyo na uwezo wa kutoa nguvu ya umeme hadi 200W,  unaotosha matumizi ya kaya nzima. Kila kifurushi kintaota paneli ya PV, betri ya nishati ya jua, taa nne za mwanga mkali,TV kubwa ya kioo cha  bapa, tochi, chagi ya simu na redio ambayo unaweza kuichagi. Vifaa hivi vinapatikana na waranti, huduma ya kufungiwa bure, huduma ya wateja na huduma ya marekebisho kwa miaka 3.  Pia, Kwa kuongezaTsh 8,999 kwamwezikwakifurushi, watejawatawezakupatahudumazaZuku TV kwamudawamasaasabakwasiku .



Akizungumza katika uzinduzi  huo   Afisa masoko wa Mobisol Sjors Martens alisema kuwa wao wanania ya kuleta maisha mazuri kwa wateja wao nchini Tanzania. 
Alisema Huduma yao  ya kifurushi cha televisheni ya satellite kitawezesha wateja  kufurahia habari , michezo, burudani na maudhui ya elimu wakati wowote hata wakiwa wanaishi  mjini au vijijini.



Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Zuku Tv Tanzania  , Bw.Omari Zuberi alisema ubunifu wa huduma hii itatuwezesha kufikia zaidi ya watanzania million 8 ambao hawajawa na nishati ya umeme wa grid ya Taifa na kutuwezesha kuchangia kwa asilimia kubwa ongezeko la televesheni nchini. 

  “Hii ni fursa ya kipekee na ya kuleta hamasa  kwa wateja wa Mobisol kuwa na uwanja mpana zaidi  wa kuchagua na kufurahia zaidi ya chaneli 40 za Zuku TV inayotambulika kama huduma bora ya bei nafuu inayotoa burudani kwa  familia kwa kuhamasisha  maudhui ya kinyumbani zaidi,” alisema Zuberi.



Aliongeza kuwa Ingawa asilimia 70 ya watanzania hawajafikiwa na huduma ya nishati ya umeme na asilimia kubwa ya watanzania bado hawana Televisheni, Mobisol na Zuku wametumia fursa hii na kuungana pamoja kwa ajili ya kutoa huduma ya umeme wa jua na kutoa burudani ya TV Satellite yenye ubora wa kimataifa



 Aidha alisema kuwa Huduma hii ya PayTV  iliozinduliwa mkoani hapa itapatikana katika mikoa ambayo Mobisol inatoa huduma ambapo ni Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Singida, Tabora, Dodoma, Mwanza, Shinyanga, Geita, Mara, Kagera, Simiyu, Mbeya, Songwe na Njombe - na baadaye kote nchini mwaka ujao



Alibainisha kuwa Kupitia Zuku TV, watanzania wanaweza kufurahia idadi ya channel  za kusisimua ikiwa ni pamoja na channel  za nyumbani  FTA, channel  za kimataifa na channel za  Zuku asili; Zuku Sports, hivi karibuni ilizindua tena  Zuku Swahili, Zuku Kids, Zuku Life Glam na Zuku Nolly.



Alisema kuwa Bei ya kifurishi cha Zuku smart pack kitakuwa kikiongezwa kwa awamu katika mfumo nishati ya  jua  ya Mobisol, ambayo wateja hulipa kupitia  simu  kwa kipindi cha miaka mitatu.

Alifafanua kuwa  Baada ya miaka mitatu, wateja watamili hivyo vifaa  na kupata ofa ya kuvutia kwa kulipa tena huduma hiyo mpya

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa