Meneja wa Benki ya KCB tawi la Arusha TFA Hogla Laizer akizungumza katika
Halfa ya Makabidhiano ya msaada wa hundi ya shilingi milioni 48 kwa shirika la Ereto East Africa foundation.Halfa ya Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi za Benki hiyo zilizopo jijini Arusha.kushoto ni Mkurugenzi wa shirika hilo Godsave Ole Megiroo
Halfa ya Makabidhiano ya msaada wa hundi ya shilingi milioni 48 kwa shirika la Ereto East Africa foundation.Halfa ya Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi za Benki hiyo zilizopo jijini Arusha.kushoto ni Mkurugenzi wa shirika hilo Godsave Ole Megiroo
Na Woinde Shizza,Arusha.
Benki
ya KCB nchini Tanzania imetoa msaada wa kiasi cha fedha cha shilingi
Milioni 48 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya kunawa mikono
vinavyojulikana kama Hand washing station katika shule za Mairowa Intergrity na Kondoa Intergrity zilizoko chini ya taasisi ya Ereto East Africa Foundation.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika ofisi za benki hiyo ,Meneja wa Benki hiyo Tawi la Arusha Hogla
Laizer amesema kuwa msaada huo ni moja kati ya mchango wa benki hiyo
kwa jamii hususan katika suala la elimu na afya hasa katika maeneo yenye
changamoto kubwa ya maji .
Meneja
huyo amesema kuwa msaada huo tayari umezisaidia shule za Kondoa
Intergrity na Mairowa Intergrity zilizoko chini ya Ereto East Africa
Foundation .
“Katika
kuchangia elimu Benki ya KCB kwa kipindi cha miaka mitatu imetoa
misaada ya thamani ya shilingi milioni 300 ili kuboresha elimu kwa kutoa
madawati na vifaa vingine vya kuboresha huduma za elimu” Alisema Hogla
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation Bwana Godsave Ole Megiro
amesema kuwa msaada huo utasaidia kutatua tatizo la magonjwa ya matumbo
na kipindu pindu yanayotokana na kutokunawa mikono kwa kuanzishwa kwa
vituo hivyo vya kunawa mikono.
Godsave amesema kuwa wameweka vituo hivyo karibu
na vyoo na karibu na mabwalo ya kunawa mikono jambo ambalo limepunguza
idadi kubwa ya wanafunzi waliokuwa wakiugua magonjwa ya matumbo.
0 comments:
Post a Comment