Nteghenjwa Hosseah, Arusha
Wakazi
zaidi ya 27,000 wa kata ya Murriet iliyopo Jiji la Arusha wataondokana na adha
ya kutembea umbali mrefu wa zaidi ya km 15 kusaka huduma ya Afya na kujifungua
kwa akina mama baada ya Mkuu wa wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro kuzindua
ujenzi wa Kituo cha Afya kitakachogharimu zaidi ya shilingi milioni 400 katika
kata hiyo.
Kuanza
kwa ujenzi wa Kituo cha Afya kitakachokuwa cha kisasa ni kufuatia malalamiko ya
muda mrefu ya wananchi wa eneo hilo kwa Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa alipokuwa
katika ziara Mkoani Arusha hususani katika Jiji la Arusha kuwa kata hiyo yenye
wakazi hao haina zahanati wala kituo cha afya cha uhakika na kufikia hatua ya
akina mama kujifungulia nyumbani au njiani wakati wakienda katika kituo cha
Afya za Levolosi kilichopo umbali wa km 15 .
Kufuatia
malalamiko hayo ya akina mama waliokuwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali ya
kutaka kituo cha afya au zahanati,Waziri Mkuu Majaliwa aliagiza mara moja
huduma hiyo kuwafikia wananchi bila ya kuchelewa.
Mhe.
Daqarro alisema kuanza kwa ujenzi wa kituo hicho ni kufuatia jitihada za Mkuu
wa Mkoa wa Arusha,Mhe. Mrisho Gambo kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi kama vile
matofali 3, 000, mifuko ya sementi 100 na bati 100 kwa ajili ya ujenzi huo.
Alisema
na kuwataka Halmashauri ya Jiji kwa
kushirikiana na wananchi wa kata hiyo
kufanya kila linalowezekana kuhakikisha Kituo hicho cha Afya hiyo kinakuwa na
maabara, chumba cha Upasuaji pamoja
chumba cha wagonjwa wa nje sambamba na vifaa vya kisasa ili wananchi waliokuwa
katika kata hiyo kupata huduma na kuondokana na adha ya kusafiri umbali mrefu.
Naye
Mkurugunezi wa Jiji Ndg. Athumani Kihamia alisema Rais Dkt. John Magufuli katika kipindi cha kampeni aliahidi kila
kata kote nchini kuwa na zahanati au kituo cha afya cha uhakika kwa ajili
ya kusongeza huduma ya afya kwa wananchi hivyo Jiji la Arusha limeanza
kutekeleza Ahadi hiyo .
Mganga
Mkuu wa Jiji la Arusha Dr. Bakari Salumu alisema kuwa Jiji la Arusha linaupungufu
wa vituo vya Afya 9 na zahanati 11 kwani vilivyopo havikithi mahitaji ya
wananchi kwa sasa.
Dr.
Bakari aliongeza kuwa kwa sasa Jiji la
Arusha lina zahanati 71 na vituo vya afya 16 mahitaji ambayo bado hayakithi
matwaka ya wakazi wa Jiji hilo lenye mitaa 154 ambalo linakuwa siku hadi siku.
Alisema
Kituo hicho cha Afya kinachojengwa kitakuwa na vifaa vyote muhimu na madaktari
wa kutosha kutoa huduma hiyo kwani kata hiyo ndio yenye wakazi wengi kuliko
kata yoyote katika Jiji la Arusha.
0 comments:
Post a Comment