Home » » Mimi ndiye Rais nipeni ushirikiano- Dkt. Magufuli

Mimi ndiye Rais nipeni ushirikiano- Dkt. Magufuli

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



na Godfriend Mbuya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watanzania kumpa ushirikiano na kuondoa tofauti zao za vyama, dini na makabila.
Rais amerejea kauli yake hiyo katika hotuba yake mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza na wananchi katika maeneo ya Arusha na Manyara ambapo amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia maendeleo.
''Uwe unataka uwe hutaki Magufuli ndiye Rais na asitokee mtu akajifanya anapingana na serikali ya Magufuli atashindwa yeye''- Amesema Rais Magufuli.
Rais amesisitiza kwamba wafanyabiashara ambao wanaficha sukari ili serikali ionekane imeshindwa kutekeleza wake ni kufanya uhujumu na serikali yake haitalifumbia macho suala hilo.
Aidha Rais amewataka viongozi wa serikali kutenga muda wa kusikiliza kero za wananchi ili kuweza kuzishughulikia kuliko kusubiri hadi yeye azunguke na kukutana na kero nyingi za wananchi.
''Uongozi ni msalaba ndugu zangu, hata mimi nisingependa kusimama hapa muda wote nikisikiliza haya kwa sababu mengi yapo juu ya uwezo wenu, fanyeni kazi kwa maendeleo ya wananchi.''
Hata hivyo Rais ameweka bayana kwamba aliahidi kuwatumikia wananchi wa chini na hakuchaguliwa na matajiri hivyo atafungamana na wananchi hao kuhakikisha kero zao zinatatulika.




0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa