Arusha
Home » , » Mkurugenzi wa Jamii Media Group Bi. Pamela Mollel Atoa Msaada kwa Wazee wa Kimandolu, Jijini Arusha

Mkurugenzi wa Jamii Media Group Bi. Pamela Mollel Atoa Msaada kwa Wazee wa Kimandolu, Jijini Arusha

Mkurugenzi wa Jamii Media group ,Pamela Mollel akikabidhi msaada wa mahitaji ya kibinadamu kwa  wazee waishio kata ya Kimandolu jijini Arusha ,anayepokea ni  Mwenyekiti wa Baraza la wazee mtaa wa kimandolu Emmanuel Mollel   ,Kata ya Kimandolu ina jumla ya wazee 400 ambao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa huduma za afya,lishe duni na huduma za kijamii.



Mkurugenzi wa Jamii Media group ,Pamela Mollel akifafanua jambo kwa wazee wazee waishio kata ya Kimandolu jijini Arusha  alipofika kuwatembelea na kutoa msaada wa kibinadamu.Kata ya Kimandolu ina jumla ya wazee 400 ambao wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa huduma za afya,lishe duni na huduma za kijamii.Picha na Ferdinand Shayo


Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog,Arusha.

Wazee waishio kata ya Kimandolu wilaya ya Arusha mkoani Arusha wamemuomba Rais John Pombe Magufuli awakumbuke wazee kwa kuhakikisha kuwa wanapata huduma bora za afya ,lishe bora na kupata mafao ya uzeeni kutokana na mchango wao katika ujenzi wa taifa kupitia sekta binafsi na za serikali tangu nchi ipate uhuru.

Wazee hao ambao wanaishi katika hali ngumu za kimaisha na wengine kutokua na uhakika wa milo mitatu huku wakikabiliwa na jukumu la kulea familia zao pamoja na wajukuu licha ya uzee unaowakabili pamoja na kutokua na kipato cha uhakika na wengine kutokua na nguvu ya kufanya kazi.

 Amon Mwita  ni mzee anayeishi kata ya Kimandolu alisema kuwa  licha ya mchango wao katika uchumi wa nchi na maendeleo ya taifa tangu kipindi cha uhuru wamekua ni watu wa kusahaulika jambo ambalo linawafanya waiishi maisha ya  shida.

Mwita alisema kuwa kwa muda mrefu wamekua wakipigwa danadana juu ya kupatiwa matibabu bure hali ambayo imesababisha afya za wazee wengi kuzoroto kwani wengine hukosa fedha za matibabu na kujikuta wakipoteza maisha kwa kukosa matibabu.

Navoneiwa Maeda ni mzee ameitaka  Serikali iwathamini wazee kwani ni kundi linaloishi katika mazingira magumu na bado halijapewa kipaumbele na serikali jambo ambalo linawaumiza hivyo ameiomba serikali na jamii ichukue jukumu la kuwalea wazee na kuwatunza.

Mwenyekiti wa Baraza la wazee mtaa wa kimandolu Emmanuel Mollel asema kuwa wazee wengi wamekua wakijificha majumbani ingali wagonjwa bila kupata matibabu na wengine kutopata mlo wa siku kutokana na hali ngumu za kiuchumi walizonazo hivyo ameiomba jamii ijitokeze kuwasaidia wazee.

Mkurugenzi wa Jamii Media Group Pamela Mollel na Mdau wa wazee Amedeus Moshi  waliofika kuwatembelea wazee  hao na kutoa msaada wa kibinadamu wameitaka jamii itambue wajibu wake wa kuwalinda na kuwatunza wazee pamoja na kukemea mauaji ya vikongwe suala linalochafua taswira ya taifa na kuathiri ustawi wa wazee nchini.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa