Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgombea
wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe
Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika
katika uwanja wa Sheikh Amri Abeis jijini Arusha wakati akiwaomba
wananchi wa jiji hilo kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka
huu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika nchini
kote na kushirikisha vyama mbalimbali vya kisiasa.
Amesema
Mara atakapochaguliwa na kuongoza taifa la Tanzania serikali yake
itamuenzi Wazriri Mkuu wa zamani kutoka jimbo la Monduli Mzee Edward
Moringe Sokoine katika kupambana na Rushwa ambapo mzee huyo hakupenda
kabisa watu ambao ni wala rushwa na wabadhirifu wa mali ya umma
serikalini alipambana kufa na kupona ili kuwasaidia wananchi
waliowanyonge.
Katika
mkutano huo pia wanachama kadhaa waliokuwa viongozi wa Chama cha
Demokrasia na Mendeleo CHADEMA wamejiunga na chama cha Mapinduzi CCM na
kutangaza rasmi katika mkutano huo, wanachama hao ni Japhet Sironga
aliyekuwa Mwenyekiti Chadema wilaya ya Monduli na Jeremiah Mepukori
Mwenyekiti BAVICHA wilaya ya Monduli ambapo wamekabidhi kadi zao kwa Dk.
John Pombe Magufuli na kadi hizo kukabidhiwa kwa Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-ARUSHA)
Mgombea
wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe
Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia katika mkutano huo wa
kampeni uliofanyika jijini Arusha leo.
Umati wa wananchi waliofurika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Kattibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Arusha
katika mkutano wa kampeni wa mgombea wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Kattibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Arusha
katika mkutano wa kampeni wa mgombea wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mjumbe wa kamati ya ushindi ya CCM Ndugu Christopher Ole Sendeka akimnadi Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
Ni Full Nyomi tu Aursha.
Msanii Ali Kiba akitumbuiza katika mkutano huo.
Dk.
John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
wakiwa wamekaa meza kuu wakati mkutano huo ukiendelea jijini Arusha
kutoka kulia ni Ndugu Christopher Ole Sendeka na Michael Lekule Laizer
Kindi la TOT likitumbuiza katika mkutano huo uliofanyika jijini Srusha.
Dk.
John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
wakicheza muziki mara baada ya kuwasili kwenye mkutano katika uwanja wa
Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Dk.
John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
wakimsikiliza mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya kampeni CCM Ndugu
Christopher Ole Sendeka.
Baadhi ya akina mama wa kimasai wakiwa katika mkutano wa kampeni mjini Monduli.
Magufuli hapa kazi tu.
Dk. John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakiteta jambo walipkutana Longido.
Jeremiah Mepukori aliyekuwa Mwenyekiti BAVICHA wilaya ya Monduli
akikabidhi kadi yake kwa Dk. John Pombe Magufuli huku Japhet Sironga
aliyekuwa Mwenyekiti Chadema wilaya ya Monduli mwenye kofia akifurahia
baada ya wote kujiunga na CCM jijini Arusha leo.
Arusha ni Magufuli tu leo.
Wasanii mbalimbali wakiimba wimbo maalum kwa ajili ya kampeni za Dk. John Pombe Magufuli uliozinduliwa leo jijini Arusha.
Wasanii wakiimba wimbo huo.
Mgombea
wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe
Magufuli akiwana viongozi mbalimbali wakiwa katika jukwaa kuu kwenye
mkutano huo jijini Arusha.
Yamoto Band wakafanya mambo makubwa sana Sheikh Amri Abeid.
Wabunge
wanaogombea ubunge viti maalum mkoa wa Arusha CCM Viola Mfuko na
Catherine Magige wakiwatunza vijana wa Yamoto Band wakati walipokuwa
wakitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni wa CCM jijini Arusha.
Mgombea
wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe
Magufuli akiwaaga wananchi wa jiji la Arusha mara baada ya kuwahutubia
kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini
Arusha.
0 comments:
Post a Comment