Home » » KITUO CHA RADIO 5 CHASHINDA NAFASI YA KWANZA MAONYESHOA YA NANENANE ARUSHA‏

KITUO CHA RADIO 5 CHASHINDA NAFASI YA KWANZA MAONYESHOA YA NANENANE ARUSHA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
SAM_4950Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera Mahusiano na Uratibu Dkt.Mary Nagu akiwa anamkabidhi kikombe Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya mara baada yakituo cha Radio5 kutangazwa washindi wa kwanza kwa upande wa Radio na wapili katika sekta nzima ya mawasiliano katika kilele cha sherehe za sikukuu ya Wakulima nanenane na maonyesho ya kilimo Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika uwanja wa maonyeshoThemi Mkoani Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_4952Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya wa Radio 5 akiwa ameshikilia kikombe walichoshinda katika maonyesho ya nanenane
SAM_4977Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya akiwa na timu yake ya ushindi mara baada ya kituo hicho kutangazwa washindi wa kwanza kwa upande wa Radio na wapili katika sekta nzima ya mawasiliano katika kilele cha sherehe za sikukuu ya Wakulima nanenane na maonyesho ya kilimo Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika uwanja wa maonyeshoThemi Mkoani Arusha
SAM_4970Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya wa Radio 5 akiwa anamkabidhi funguo ya pikipiki kwa Mkuu wa wilaya Monduli Jowika Kasunga zawadi ya mshindi wa kwanza katika kilimo
MAKUNDIKushoto ni Rais wa Taasisi ya upendo kwa mama Eng.Carlos Mkundi akiwa katika banda la Radio 5 na DJ Haazu ambapo Taasisi ya upendo kwa mama wamedhamini maonyesho ya nanenane kupitia kituo cha Radio 5

UPENDO KWA MAMA
SAM_4974
Wafanyakazi wa Radio 5 katika nyuso za furaha

Kituo cha Radio 5 kilichopo jijini Arusha kimeshika nafasi ya kwanza katika maonyesho ya nanenane kwa upande wa Radio na wapili katika sekta nzima ya mawasiliano katika kilele cha sherehe za sikukuu ya Wakulima nanenane na maonyesho ya kilimo Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika uwanja wa maonyeshoThemi Mkoani Arusha

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kikombe na mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera Mahusiano na Uratibu Dkt.Mary Nagu Meneja masoko na mawasiliano Sarah Lazaro Keiya alisema kuwa wanafuraha kubwa kwa kupata ushindi huo

Alisema kuwa Radio 5 imekuwa ikiwapa kipaumbele wakulima ambapo wamekuwa wakiandaa vipindi vya kilimo ambapo katika studio zao huwaalika wataalamu mbalimbali wa kilimo lengo ni kuwapa elimu kuhusu kilimo cha kisasa
Pia Radio hiyo imekuwa ikiwapatia wakulima msaada wa mbegu,mbole na wamekuwa wakiwatembelea mara kwa mara kujua maendeleo yao katika masuala ya kilimo
“Vipindi vyetu vya kilimo vimekuwa vikitupa tuzo mbalimbali nah ii leo katika maonyesho haya pia tumepata tuzo”alisema Keiya
Aidha alisema kuwa wamekuwa wakitoa zawadi kila mwaka kwa mkulima bora atakayechaguliwa na TASO ambapo wametoa pikipiki aina ya powew king yenye thamani ya shilingi milioni mbili,mbole pamoja na mbegu
Hata hivyo alitoa shukrani zake kwa mkurugenzi wa kituo hicho Bw,Robert Francis kwa kuwawezesha wafanyakazi kufanya vizuri katika maonyesho hayo huku akisema kuwa anatimu nzuri inayojituma na yenye uwezo mkubwa kikazi
Aliwashukuru wadhamini SBs(pepsi),Kishen enterprises limited,Upendo kwa mama foundation,Grandmaster records,Atown records na wote waliojitokeza kushirikiana nao
    

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa