Home »
» MUSTAFA PANJU AJINADI KWA WANANCHI WA JIMBO LA ARUSHA ASEMA AKIPATA UBUNGE HAWATAJUTIA KAMWE
MUSTAFA PANJU AJINADI KWA WANANCHI WA JIMBO LA ARUSHA ASEMA AKIPATA UBUNGE HAWATAJUTIA KAMWE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa
Panju ambaye ni mmoja wa wagombea wa jimbo la Arusha mjini kupitia chama
cha mapinduzi CCM akiongea katika mkutano wa hadhara katika kata mpya
ya Olmoti jana ambapo wagombea 12 walipata fursa ya kujitambulisha kwa
wananchi na kunadi sera zao,
Mustapha panju amesema kuwa kilicho msukuma kugombea nafasi hiyo ni
kuakikisha wananchi wa jimbo la arusha wanapata ridhaa ya kuwa na
maendeleo ya hali ya juu ikiwemo kuweza kukua kisayansi na kuweza
kufika mwezini.(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mustafa
Panju akiwa na wagombea wenzake wa chama hicho jana katika kata mpya ya
Olmoti jijini Arusha walipokwenda kujitambulisha kwa wananchi na kunadi
sera zao pia walipata fursa ya kutembelea kata ya Olasiti,Osunyai JR
Mtoto
aliyefika kusikiliza sera za wagombea Ubunge wa chama cha Mapinduzi
(CCM) akiwa ameshikilia kipeperushi cha mgombea Ubunge jimbo la Arusha
Mustafa Panju katika kata ya Osunyai JR
Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano
akizungumza katika kata mpya ya Olmoti jana ambapo alisisitiza wananchi
kusikiliza sera za wagombea huku akiwataka kutokupiga makofi au
kushangilia wakati wakijieleza
Meza kuu pamoja na wagombea Ubunge jimbo la Arusha mjini
Wananchi waliokuja kuwasikiliza wagombea Ubunge jimbo la Arusha mjini wakiwa makini kusikiliza,
0 comments:
Post a Comment