Home » » WAKULIMA WAWALALAMIKIA WAFANYABIASHARA

WAKULIMA WAWALALAMIKIA WAFANYABIASHARA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


WAKULIMA wilayani hapa wamewalalamikia wafanyabiashara  na madalali wanaotumia vipimo vya lumbisa katika upimaji wa mazao yao.

Wakulima hao wameiomba serikali kuingilia kati upimaji  wa vipimo hivyo ili kuweza kuwanyanyua wakulima ambao wamekuwa wakididimizwa kila mwaka na wafanyabiashara kwa manufaa yao.

Wakulima hao walisema hayo wakati wakiwa kwenye mkutano wao wa Mtandao wa Wakulima (MVIWAKA) uliofanyika mwishoni mwa wiki wilayani hapa ulioshirikisha wakulima kutoka kata nane za wilaya hiyo ambao walijiunga kwenye vikundi vya mtandao huo.

Katika hotuba yake mwakilishi wa mkuu wa Wilaya ya Karatu  ambaye ni Afisa tarafa ya Karatu Bw. Paskali Ng'adi alisema kuwa serikali ilikwisha piga marufuku utumiaji wa vipimo mbalimbali vinavyotumiwa na wafanyabiashara ikiwemo kipimo cha lumbesa inayotumiwa na wafanyabiashara wa vitunguu.

Aliwataka wakulima hao kutoa taarifa ofisi ya wilaya kwa mfanyabiashara yeyote atakayetumia vipimo visivyotakiwa  na serikali ili kuweza kuchukuliwa hatua za kisheria.

Pia Bw.Ngadi aliwataka wakulima ambao bado hawajajiunga kwenye vikundi vya mtandao huo kujiunga ili kuweza kutatuliwa matatizo yao kwa urahisi na pia kuweza kupata mikopo inayotolewa na serikali katika kujiinua kiuchumi.

Kwa upande wake mratibu wa MVIWATA Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Masandika alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa  mtandao huo wa wakulima wilayani Karatu (MVIWAKA) ni kuweza kuwasaidia wakulima ambao wamekuwa wakilima kilimo kisicho na tija na kukosa masoko ya uhakika ndani ya nchi na nje.
 
Alisema kuwa sambamba na masoko pia mtandao huo huwaunganisha wakulima na taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi na pia kuwatatulia matatizo yao kiurahisi kwa wakulima walioko ndani ya mtandao.

Chanzo:Majira

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa