Arusha
Home » » MUNISl ASHAURI WAGOMBEA CCM KUTOCHAFUANA‏

MUNISl ASHAURI WAGOMBEA CCM KUTOCHAFUANA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
SAM_2935
Pichani ni Mgombea anayetajwa kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Arusha mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),Thomas Munisi (Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

Mgombea anayetajwa kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Arusha mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),Thomas Munisi amewataka wagombea wa chama hicho kutochafuana kwenye majukwaa na vijiwe bali wafanye kampeni za kistaarabu.

Munisi,ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Kilimanjaro Millenium Printers(KPML) yenye makao makuu yake jijini Arusha alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa kuhusu uamuzi wake wa kugombea ama la.
Hadi sasa jijini Arusha jumla ya wagombea saba wamejitokeza kutia nia ya kugombea jimbo la Arusha mjini kupitia CCM ambao ni Kim Fute,Mustapha Panju”Bushbuck”,Phillemon Mollel”Monaban”,Victor Njau,Edmund Mgemela,David Rwenyagira pamoja na mbunge wa zamani wa jimbo hilo Felix Mrema.

Akiongea katika hoteli ya Palace iliyopo jijini Arusha alisema kuwa si vyema wagombea wa CCM kuanza kampeni za kuchafuana kupitia kwenye vijiwe na majukwaa kwa kuwa haileti picha nzuri ndani ya chama.

“Mimi nashangaa wagombea wanapita huko vijiweni na kuanza kuchafua wenzao wakati sote tunajenga nyumba moja”alisema Munisi ambaye pia ni mmiliki wa kamuni ya madini ya Tom Gems

Hatahivyo,alisema kuwa ndani ya CCM watajitokeza wagombea mbalimbali lakini mwisho wa siku ni mgombea mmoja tu atakayepitishwa na chama kwa lengo la kupeperusha bendera ya CCM.

Akizungumzia uamuzi wake wa kugombea jimbo hilo au la alisema kuwa kwa kuwa taratibu ndani ya chama zimeshatangazwa na muda ukiwadi atafanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya wakazi wa jimbo la Arusha mjini.

    

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa