Home » » BODI YA NHC YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA UJENZI WA NYUMBA JIJINI ARUSHA

BODI YA NHC YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA UJENZI WA NYUMBA JIJINI ARUSHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Ujumbe wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC ukiwa eneo linalomilikiwa na  NHC ambalo ujenzi wa Mji wa kisasa umeanza wakionyeshwa na Meneja wa NHC Mkoa wa Arusha Bw. James Kisarika chemchemu za maji yanayotiririka walipotembelea eneo hilo lenye hali ya hewa ya aina yake Jijini Arusha jana.

Usariver ni Arusha Tanzania ambapo NHC Shirika lenye dhamana ya kujenga nyumba bora hapa nchini limeanza kupanga mji huo wenye mandhari na hali ya hewa ya kuvutia. Hapa wajumbe wa Bodi ya NHC na watendaji wa NHC wanafurahia mpango wa kuendeleza eneo hilo lenye ekari 300 linalomilikiwa na NHC.


Hii ndiyo hatua ya ujenzi iliyokwishafikiwa hivi sasa katika ujenzi wa nyumba za gharama ya kati aina ya “town houses” zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli kwa ajili ya watumishi wa Halmashauri hiyo.


Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Bw. Haikamen Mlekio akitoa maelezo ya awali kwa Makamu Mwenyekiti wa NHC Bw. Deo Mmari na wajumbe wengine wa Bodi, ya utekelezaji wa ujenzi wa nyumba za gharama ya kati aina ya “town houses” zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli kwa ajili ya watumishi wa Halmashauri hiyo.


Msimamizi wa mradi wa nyumba za gharama ya kati zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli Bw. Hassan Bendera(kushoto) akitoa maelezo kwa Makamu Mwenyekiti wa NHC Bw. Deo Mmari(mwenye suti nyeupe), ya hatua za ujenzi zilizofikiwa katika mradi wa nyumba za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli zinazojengwa na NHC


Meneja wa NHC Mkoa wa Arusha Bw. James Kisarika akitoa maelezo kwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC Bw. Deo Mmari ya viwanja vilivyotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ambavyo hivi karibuni vitajengwa  nyumba za gharama nafuu. Eneo hili limepewa NHC na Halmashauri hiyo kama sehemu ya kulipa gharama zilizotokana na NHC kuijengea Halmashauri hiyo nyumba za watumishi wake.


Meneja wa NHC Mkoa wa Arusha Bw. James Kisarika akitoa maelezo ya mpango wa uendelezaji mji wa kisasa wa Safari City ulioko Mateves nje kidogo ya Jijini Arusha mbapo hivi karibuni NHC itaanza ujenzi wa nyumba 300 za gharama nafuu za kuuzia wananchi.


Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC Bw. Deo Mmari na Wakurugenzi wengine wa Bodi wakijadili jambo kuhusu mpango mji uliyowekwa na NHC katika uendelezaji wa mji mpya wa Safari City wenye ekari 600 alipotembelea eneo hilo lililopo Mateves nje kidogo ya Jiji la Arusha jana.


Meneja Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa nyumba na vivutio mbalimbali katika eneo la NHC Usariver Bw. Muradi Yusufali akiwatembeza Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC katika mradi wa ujenzi wa mji wa kisasa Usariver walipotembelea eneo hilo jana. Ukamilishaji taratibu kadhaa za ujenzi wa nyumba katika eneo hilo na ujenzi wake umeshaanza.
Meneja wa NHC Mkoa wa Arusha Bw. James Kisarika akiwapa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi maelezo na mpango wa uendelezaji wa mji wa kisasa eneo la Usariver lenye vivutio kadhaa walipotembelea eneo hilo  lenye ekari 300 jana.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa