Arusha
Home » » Arusha Ryno washindwa kuwatambia Mombasa SC nyumban

Arusha Ryno washindwa kuwatambia Mombasa SC nyumban

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

wachezaji wa Arusha ryno (Tanzania- kijani) wakiwania mpira uliorushwa pamoja na timu ya Mombasa sc


Timu ya Arusha Ryno ya Tanzania imeshindwa kutamba nyumbani mbele ya timu ya Mombasa SC ya Kenya, baada ya kulazwa kwa point 28-26 katika mchezo wa awali wa mfululizo wa mashindano ya Rugby yanayoshirikisha timu za nchi za Afrika mashariki.
Arusha Ryno ilishindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani wa TGT ulioko kisongo jijini Arusha kwa mara ya kwanza mbele ya Mombasa katika michuano hiyo ya mchezo wa Rugby ya nchi za Afrika mashariki ijulikanayo kama “Hatch cup” iliyochezwa mapema mwishoni mwa wiki.
Timu ya Arusha ryno wakimiliki mpira
Akizungumza baada ya michuano hiyo, Kaptein wa timu ya Arusha Ryno, Justine Robert alisema kuwa tangu kuanza kwa mashindano hayo kwa zaidi ya miaka mitatu hawajawahi kufungwa na timu ya Mombasa lakini kwa leo hali hiyo imetokea hali inayowatia uchungu sana na kuahidi kufanya vizuri katika mechi ya marudiano.
“Kiukweli hatujawahi kufungwa na hawa jamaa lakini imetokea hivyo niahidi kwa sababu ni mechi ya awali na kuna marudiano tutafanya vema na tutaanza mazoezi makali kwa ajili ya kuwafunga mabingwa watetezi ambao ni “Dar-es-salaam Leopard” may 9 mwaka huu hivyo mashabiki wetu wasikate tama kwani kombe hili la “Hutch cup” linakuja Arusha”
Kwa upande wake kaptein wa timu ya Mombasa SC, Chris Atingo alisema kuwa wanayo furaha kwa mara ya kwanza kumfunga timu ya Arusha Ryno kwani kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa vibonde mbele ya timu hiyo hali iliyowalazimu kufanya mazoezi ya usiku na mchana kuhakikisha wanakuwa mlima mkali.
“Leo tunayo furaha kumfunga Arusha kwani miaka kadhaa sasa wamekuwa wakitufunga hali ambayo imefikia sehem tukasema iwe mwisho na tukaamua kufanya mazoezi usiku na mchana na matunda ya mazoezi yetu tumeyaona na tutaendelea ili kumfunga pia dar- Leopard na Arusha tutakapomkaribisha nyumbani kwetu Mombasa hivyo karibuni na ninyi waandishi muone vibonde wamegeuka mlima” alisema Chris wakishangiliana na timu wenzake.
Aidha michuano hiyo ya mchezo wa Rugby inayohusisha nchi za Afrika mashariki kwa mwaka huu zimeshiriki timu tatu za Dar, Arusha na Mombasa yakiwa na malengo ya kuwafanya vijana chipukizi kuwaonesha mbinu za mchezo huo katika mashindano ili waweze kuiga na kuyatekeleza ili kushinda wanaposhiriki katika mashindano ya kimataifa ambapo timu za nchi hizi zimekubaliana kushirikiana kukuza mchezo huu.
 
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa