Lowassa ambaye alirejelea kauli yake ya kwamba yeye si tajiri bali ni
tajiri wa marafiki, alichangia shilingi milioni tatu kwa ajili ya sare
za shule kwa wanafunzi ambao nguo zao ziliteketea.
Aidha mwenyekiti mtendaji wa makampuni IPP, Reginald Mengi akichangia
shilingi milioni 25 kwa ajili ya vitanda na Kampuni ya A to Z ikichangia
ujenzi wa mabweni mawili yaliyo ungua moto hivi karibuni.
Mmiliki wa kiwanda kikubwa cha A to Z cha Arusha,Anoji Shah (aliesimama)
akiwaeleza wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Engutoto
wilayani Monduli umuhimu wa elimu na pia kutangaza msaada wa ujenzi wa
mabweni yote mawili yaliyoteketezwa kwa moto wiki mbili zilizopita.
Mbunge wa Monduli na waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa akizungumza
wakati alipotembelea shule ya sekondari ya wavulana ya Engutoto wilayani
Monduli, mkoani Arusha jana. Mbunge huyo alichangia shilingi milioni 3
kwaajili ya sare za wanafunzi zilizoungua wakati wa ajali ya moto
shuleni hapo. Kampuni ya Ato Z wameahidi kujenga mabweni mawili ya shule
hiyo yaliyounga na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi
aliyechangia shilingi Milioni 25 kwa ajili ya ununuzi wa vitanda.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment