Na
Mwandishi Wetu, Arusha
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniella Schadt ametoa wito kwa jamii
kuhakiksha wanatoa kipaumbele katika kushirikisha vijana kwenye nyanja
mbalimbali za maendeleo.
Wito huo umetolewa juzi
jijini Arusha wakati Mke huyo wa Rais wa Ujerumani alipokuwa akizindua mradi wa
utetezi na ushawishi wa jamii katika kutoa vipaumbele katika sekta za Elimu,
Afya na Ajira kwa vijana ujulikanao kama BEYOND 2015 ambapo mradi huo
unaratibiwa na Shirika lisilo la Kiserikali la DSW Tanzania.
Bibi. Daniela alisema
kuwa jamii inapaswa kutoa mkazo katika sekta za Elimu, Afya na Ajira kwa vijana
kwa kuwa duniani kote vijana ndiyo nguvu kazi katika kuletea maendeleo ya taifa
lolote lile.
‘Tunapaswa kuweka mkazo
kwa vijana wadogo, maisha yao ya baadaye yanaanza kuanzia sasa, tuweke mkazo
katika Elimu na Afya kwa vijana wetu ili waeze kutambua fursa na kuzitumia.’’
Alisema Bibi. Daniela.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa DSW Tanzania Bwana Peter Owaga amesema kuwa ni wao kama asasi ya kirai
wanashirikia na Serikali katika kuhakikisha utekelezaji wa sera zinazohusu
vijana nchini zinaleta tija
Owaga ameongeza kuwa
Serikali kama msimamizi imepiga hatu kubwa kwa kuwa na Sera na miongozo mbalimbali
inayohusu vijana kama vile Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 inayotoa
fursa kwa kijana kujitambua.
Aidha Owaga aliongeza
kuwa mradi wa BEYOND 2015 ambao umezinduliwa na Mke wa Rais wa UjerumaniBibi.
Daniela Schadt umelenga kuongeza ushawishi na hamasa kwa washirika wa maendeleo
ili kutoka kipaumbele kwa kutenga bajeti kwa ajili ya Elimu , Afya ya Uzazi na
Ajira kwa vijana.
Akizungumzia mikakati
na namna mradi huo utakavyotekelezwa Afisa Muhamasishaji na Mawasiliano Bi.
Ester Mwanjesa amesema kuwa mradi huo utatekelezwa kwa mwaka mmoja katika mikoa
yote nchini ambapo mijadala mbalimbali itakuwa ikifanyika ili kuongeza hamasa
ya uashawishi utakaopelekea kutoa kipaumbele kwa vijana hususan katika nyanja
za Elimu, Afya ya uzazi na Ajira.
Mradi huu wa BEYOND
2015 ambao ni kifupi cha maneno Building
Expert Youth and Organisation for National Postion on the Post 2015 Development
umelenga kutatua changamoto za vijana asa baada ya kumalizika kwa muda wa
Malengo ya Melenia mapema mwaka huu.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment