Arusha
Home » » MALIMA ‘AWAFUNDA’ WATAALAMU WA MANUNUZI

MALIMA ‘AWAFUNDA’ WATAALAMU WA MANUNUZI

NAIBU Waziri wa Fedha, Adamu Malima ametaka wataalamu wa manunuzi na ugavi kusema ukweli kwa faida ya nchi. Malima alisema hayo jana wakati akifungua mkutano wa wataalamu hao jijini hapa.
Waziri Malima alisema katika bajeti ya serikali asilimia 65 iko katika manunuzi ya umma na iwapo wataalamu wa idara hiyo hawatakuwa makini upo uwezekano mkubwa wa uchumi wa nchi kuyumba.
Waziri Malima alisema kwa sasa taaluma ya manunuzi na ugavi katika sekta binafsi na umma hairidhishi hivyo Bodi ya Wataalamu inapaswa kufanya kazi yake kwa umakini na kupamba na hilo kwa maslahi ya taifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi (PSPTB), Clemence Tesha alisema kwa sasa taaluma hiyo imekuwa katika wakati mgumu kwani baadhi ya vifaa nchini havina ubora unaokidhi mahitaji .
Mjumbe wa Bodi ya PSPTB, Dk Hellen Bandiho alitaka serikali, taasisi za umma na binafsi kuacha kuajiri wataalamu wa manunuzi na ugavi wasiosajiliwa na Bodi hiyo kwani kwa kufanya hivyo ni kukiuka kanuni na sheria za kazi.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Chanzo;Habari Leo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa