Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WATUHUMIWA
19 waliokamatwa na Jeshi la Polisi jijini Arusha wakihusishwa na
matukio mbalimbali yanayoashiria ugaidi, ikiwemo milipuko ya mabomu na
umwagiaji tindikali, wanatarajiwa kupanda kizimbani leo katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi jijini hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi (ACP), Liberates
Sabas, alisema jana kwamba kati ya watuhumiwa hao ni pamoja na Sheikh wa
Msikiti Mkuu, Mustafa Kihago (46), na Imamu wake Abdul Azizi (49),
ambao wote kwa kushirikiana na watu wengine wanatuhumiwa kuhusika na
mlipuko wa bomu uliotokea nyumbani kwa Sheikh Abdul Jonjo na kumjeruhi
katika eneo la Esso jijini hapa Oktoba 25, 2012.
Wengine wanaohusika na tuhuma hizo ni Yusuph Huta (30), na Kassimu Idrisa (34).
Kamanda Sabas, alitaja watuhumiwa wengine waliokamatwa na kuhusishwa
na tukio la mlipuko wa bomu Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi eneo
la Olasiti Mei 5, 2013 kuwa ni Huta, Ramadhani Waziri (28), Abdul Humu
(30), Japhary Lema, Said Temba na Kassim Ramadhani (34). Wengine
waliodaiwa kutekeleza unyama huo ni Abdulrahmani Hassan (41), mfanyakazi
wa Benki ya Stanbic tawi la Arusha, Morris John Muha (44), Niganya
Niganya (28), na Hassan Omar (40).
Aliwataja watuhumiwa wa tukio la mlipuko wa bomu kwenye viwanja vya
Soweto kwenye mkutano wa hitimisho la kampeni ya uchaguzi wa udiwani wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na kuua watu watatu na
kujeruhi wengine kadhaa Juni 15, 2013 kuwa ni Huta (30), Humud (30),
Lema (38), na Temba (42).
Pia, aliwataja watuhumiwa wengine walioongezeka baada ya mlipuko wa
bomu katika mgahawa wa Vama kuwa ni pamoja na Kassim (34), Ramadhani
(24), Abashar Omar (24), Abdulrahman Hassan (41), Morris (44), Niganya
(28), Ntembo (40), na Hassan (40).
Akielezea tukio la kumwagiwa tindikali Sheikh Said Makamba wa msikiti
wa Kwa Morombo Julai 11, 2013 aliwataja watuhumiwa watakaofikishwa
mahakamani kuwa ni Huta (30), Ramadhan (28), Kassin Idrisa (34) na Lema
(38).
Kamanda Sabas, aliwataja pia watuhimiwa waliodaiwa kuhusika na tukio
la kumwagiwa tindikali Sheikh Kihago (49), kuwa ni pamoja na Huta (30,)
Kassim (34), Lema (38), Hassan Mfinanga (57).
Aliwataja watuhumiwa wawili walioongezeka katika tukio la mlipuko wa
bomu kwenye baa ya Arusha Night Park Aprili 13, 2014 kuwa ni Lema (38),
na Ibrahimu Leonard (37), maarufu kama Sheikh Abuu Ismail (37).
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment