Arusha
Home » » MWINGINE AONGEZWA KESI ULIPUAJI BOMU KANISANI

MWINGINE AONGEZWA KESI ULIPUAJI BOMU KANISANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

KESI ya ulipuaji bomu wakati wa uzinduzi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi lililopo Jijini Arusha Mei 5 mwaka jana na kuua watu watatu na wengine kadhaa kujeruhiwa juzi ilichukua sura mpya baada ya mtuhumiwa mwingine kuongezwa.
Mtuhumiwa huyo ambaye anafanya idadi ya washitakiwa kuwa 14 alisomewa mashitaka 21 ya kukusudia kuua na matatu ya kuua.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Augustino Kombe akisaidiwa na Felix Kwetukia aliiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha mbele ya Hakimu Devotha Msofe kumwongeza mtuhumiwa mwingine, Abdul Hassan Mussa katika shitaka hilo.
Mapema asubuhi Mussa alifutiwa shitaka la kutenda njama za kufanya ugaidi na kutoa msaada kwa vikundi vya ugaidi shitaka lililokuwa mbele ya hakimu mkazi Hawa Mguruta na kuunganishwa katika shitaka jipya la mauaji na kujaribu kuua kwa kukusudia.
Watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Mei 5 mwaka jana kinyume na kifungu namba 196 (A) cha sheria ya kanuni za adhabu namba 16 (2002) na kifungu namba 211(A) cha sheria ya kanuni za adhabu namba 16 (2002).
Aidha, Kombe aliieleza Mahakama kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja walimuua kwa bomu la kutupa kwa mkono Patricia Joachim, Regina Loning’o na James Gabriel, wote wakazi wa jijini hapa wakati wakiwa kanisani.
Chanzo;Habari Leo 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa