Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ZAIDI ya mikopo ya sh.
milioni 151 imetolewa kwa akinamama 287 kwa muda wa miaka mitatu tangu
mwaka 2012 hadi 2014 na kikundi cha Arusha Meru Women Saccos lengo ikiwa
ni kuwainua akinama kuichumi.
Hayo yalisemwa na
mwenyekiti wa kikundi hicho Bi.Eva Kaaya juzi katika maonyesho ya
Nanenane katika Viwanja vya Themi jijini Arusha.
Alisema kuwa hadi sasa
wametoa mikopo kwa akinamama zaidi ya sh.milioni 151 kwa ufadhili wa
Canadian Co-operative Association kupitia Moshi University College of
Co-operative and Business Studies.
Alisema kuwa lengo lao
hasa la kufanya hivyo ni kuwainua akinamama kiuchumi hali itakayopelekea
wao kuondokana na umaskini katika familia zao huku akiweka wazi kuwa
hadi sasa mikopo iliyorejeshwa ni sh. milioni 97,644,066 na mikopo
iliyobaki ni sh.milioni 53,735,934.
Bi.Kaaya alisema kuwa
wamekuwa wakiwahudumia akinamama kutoka Arusha na Arumeru kwa kuwapa
mikopo wajasiriamali, ambapo sharti la kupata mkopo ni lazima awe na
hisa katika kikundi hicho na kumfanya mwombaji wa mkopo awe mmiliki
halali wa Saccos.
"Ili akinamama wapate
mkopo ni lazima wawe katika kikundi cha watu watano,awe mwanachama hai
na awe na akiba kwa kufuata masharti hayo mwombaji anapewa mkopo bila ya
msharti magumu," alisema Bi.Kaaya.
Kwa upande wake katibu
wa kikundi hicho Bi. Martha Temba alisema kuwa njia mojawapo
iliyowafanya wakafika hapo ni utoaji wa mafunzo kwa akinamama juu ya
elimu ya Saccos kwa kuweka na kukopa inayotolewa na Chuo cha Ushirika
Moshi.
"Mafanikio tuliyonayo
sasa ni kutokana na akinamama kupewa elimu ya Saccos,kabla ya elimu
walikuwa wakichukua mikopo kienyeji hali iliyopelekea wengine kushindwa
kuendelea na kikundi," alisema Bi.Temba.
Aidha, alisema kuwa wapo na timu kutoka ushirika ambapo wanawafikia kina mama katika kata na vijijini na kuwapa elimu ya Saccos.
Naye Afisa Ushirika
Halmashauri Wilaya ya Arusha DC Bi.Sophia Shoko alisema kuwa majukumu
yao makubwa ni kusimamia sheria na kukagua,kuhamasisha wanachama
kujiunga katika Saccos.
Pia aliongeza kuwa kazi
yao ni pamoja na utoaji elimu ya ushirika, utunzaji wa kumbukumbu,haki
na wajibu wa mwanachama,huku akiwataka akinamama kupunguza kuwa na
mikopo mingi isiyokuwa na tija
Chanzo:Majira
0 comments:
Post a Comment