Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399
WANAFUNZI wa shule za sekondari kutoka jamii za Kimasai wamepata
fursa ya kuongeza taaluma na stadi za maisha baada ya Shule ya
Sekondari ya Orkeeswa kushirikiana na shule ya kimataifa ya Groton ya
nchini Marekani.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo iliyopo Monduli, Arusha inayosomesha
watoto kutoka familia duni, Yusuph Mollel, alisema mpango huo
umewezesha wanafunzi kwenda Marekani kujifunza katika shule ya Groton
kwa miezi mitatu.
“Ushirikiano huu umezaa matunda, wanafunzi wanaporudi wanakuwa na ari
ya kusoma na hata kufanyakazi za umma wanapokuwa nyumbani… wamejitolea
kwenda shule za jirani na kuwafundisha wanafunzi masomo mbalimbali
ikiwemo Kingereza,” alisema Mollel.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa idara ya ushauri
nasaha kutoka shule ya Groton ambaye yupo nchini na wanafunzi kutoka
Marekani, Megan Harlan alisema mpango huo umetoa fursa kwa wanafunzi
wote kufahamu masuala mbalimba ya kitaaluma.
“Wanafunzi wangu wamefurahia utamaduni wa kimasai na kufahamu kwamba
kuna tofauti kati ya utamaduni wa kimarekani na Tanzania… hii
isingekuwa rahisi bila kuwepo kwa mpango huu,” alisema.
Sophie Baker ni mwanafunzi wa Groton alisema amejifunza mambo mengi
kuhusu ukarimu wa watanzania hasa wamasai na kamwe hataisahau Tanzania
na watu wake.
Naye mwanafunzi wa kidato cha tano wa shule ya Orkeeswa aliyekwenda
Marekani, Florah Tipapurwa alisema mfumo wa elimu ya Marekani ni wa
juu zaidi ikilinganishwa na Tanzania likiwemo tatizo la ukosefu vitabu,
madawati na waalimu wa kutosha
Chanzo;Tanzani Daima
0 comments:
Post a Comment