Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WATANZANIA wameshauriwa kutumia vyakula vyenye virutubisho badala
ya kula vilivyokobolewa, hali inayochangia watu wengi kudhoofika kiafya
na kupata magonjwa ikiwemo utapiamlo.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Monaban inayojihusisha na usambazaji wa
vyakula vyenye virutubisho ndani na nje ya nchi, George Mboje, alitoa
kauli hiyo mjini hapa hivi karibuni na kusema kukosekana kwa
virutubisho muhimu katika vyakula kumekuwa kukisababishia watu
kushambuliwa na maradhi kwa urahisi.
Kutokana na hali hiyo, aliwashauri Watanzania kutumia bidhaa
zisizokobolewa zenye virutubisho, ili kujenga jamii imara yenye afya
bora itakayoleta uchumi imara kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.
“Kwa sasa wazalishaji wote wamepokea maelekezo kutoka Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA) juu ya kuongeza virutubisho kwenye vyakula, sisi
ni wadau ambao tunatekeleza maagizo hayo na kuwatendea haki walaji kwa
kuwauzia vyakula vyenye virutubisho,” alisema George.
Alisema kampuni hiyo imekuwa ikisambaza vyakula vyenye virutubisho
ndani na nje ya nchi ambavyo ni unga wa mahindi, ngano, maharage na
nafaka nyingine.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment