Arusha
Home » » TFF KUIUNGA MKONO ROLLYSTORE MASHINDANO YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KWA VIJANA YA MIAKA 20‏

TFF KUIUNGA MKONO ROLLYSTORE MASHINDANO YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KWA VIJANA YA MIAKA 20‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Bertha Mollel – Arusha.

Shirikisho la kandada nchini Tanzania (TFF) limeingilia kati kuokoa mashindano ya vijana ukanda wa maziwa  makuu ambayo yalikuwa hatihati kufanyika na sasa yataendeshwa kwa kushirikiana na waratibu wa mashindano hayo Rollingstone Sports academy ya mjini Arusha chini ya mwamvuli wa mtandao wa taasisi za za soka la vijana afrika mashariki na kati ECAYFA.

Mashindano hayo ya wazi hufanyika kila mwaka mkoani Arusha mwaka huu yatafanyika jijini dar es salaam na kushirikisha timu za vijana za under 20 na under 14 kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Kenya, ,Zanzibar, na jamhuri ya kidemokrasia ya kongo (DRC) na yatafanyika wiki ya kwanza ya mwezi julay.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mkurugenzi wa rollingstone football academy ally mtumwa masoud alisema mashindano hayo yalikuwa katika hatihati ya kufanyika au kutofanyika baada ya TFF kuchelewa kutoa kibali cha kuendesha mashindano hayo kwani taasisi hiyo iliandika barua ya kuomba kibali tangu mwezi wa pili lakini hawakupatiwa kibali kwa wakati.

Mtumwa alisema kuwa kufuatia kuchelewa kwa kibali hicho walishindwa kufanya maandalizi ya mashindano hayo ikiwa ni pamoja na kutafuta wafadhili na kualika timu hususani zile zinazotoka nje ya nchi  hali iliyosababisha kufikiria kuyasogeza mbele au kutofanyika kabisa kwa mashindano hayo.

Hata hivyo baada ya kufuatilia TFF walikiri kupokea barua hiyo na kusema sababu zilizochangia kutofanyiwa kazi kwa barua hiyo ni piikapilika za TFF kuhama ofisi kupisha ukarabati wa ofisi za karume lakini kwa kujua umuhimu na ukubwa wa mashindano hayo waliamua yafanyike kwa ushiriano wa pamoja na Rolly store kwa sharti la mashindano kufanyika jijini dare s salaam ili waweze kushuhudia.

Hii itakuwa mara ya pili kwa mashindano hayo ya 14 kufanyika nje ya Arusha kwani mwaka 2012 yalifanyika nchini Burundi na utakuwa mwanzo wa mashindano hayo kuzunguka katika mikoa na nchi mbalimbali ambazo zitakuwa tayari kuandaa na kukidhi vigezo ikiwa ni pamoja na kuhudumia malazi na chakula kwa timu zinazotoka nje ya nchi.

TFF, rollingstone na ECAYFA wameunda kamati ya maadalizi itakayokuwa chini ya uratibu wa afisa uhusiano na mawasiliano wa rollingstone Wilbrode Alfonce na tayari nchi wanachama wa CAYFA na taasisi za sika nchini Tanzania zimeshatumiwa barua za mialiko huku baadhi ya nchi kama burundi ,Kenya na DRC zikionyesha nia ya kushiriki.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa