Arusha
Home » » REDD'S MISS ARUSHA WAJIACHIA KAMBINI

REDD'S MISS ARUSHA WAJIACHIA KAMBINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Redd’s Miss Arusha wajichimbia kambiniWAREMBO 13 wa Redd’s Miss Arusha 2014 jana wameingia rasmi kambini kujinoa kwa ajili ya kinyang’anyiro kinachotarajiwa kufanyika Juni 7.
Muandaaji wa Redd’s Miss Arusha, Faustine Mwandago, alisema kuwa warembo hao ni washindi waliotokana na mashindano ya ngazi ya vitongoji yaliyomalizika hivi karibuni.
Mwandago, aliwataja warembo hao kuwa ni Janeth Alex (20), Neema Urio (19), Lilian Deus (18), Leila Thomas (19), Husna Hamis (20), Happyness Tarimo (19), Eveline Baasa (19), na Marry Joel (21).
Wengine ni Neema Charles (19), Dyness Peter (21), Rahisa Mboye (21), Joselyn Mirashi (21), na Amber Gladys (20).
Mwandago alisema kuwa shindano hilo litasindikizwa na burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii mbalimbali wa Mkoa wa Arusha, wakisindikizwa na msanii mkubwa ambaye hata hivyo hakuwa tayari kumtaja.
Taji la Redd’s Miss Arusha linashikiliwa na mrembo Glory Stephen.
Chanzo:Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa