Home » » NAIBU MEYA AMPANDA KIZIMBANI

NAIBU MEYA AMPANDA KIZIMBANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
NAIBU Meya wa Jiji la Arusha, Prosper Msofe na Diwani wa Kata ya Levelos, Ephata Nanyaro, wote kutoka CHADEMA, wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kumshambulia mgambo wa jiji, William Mollel.
Mwanasheria wa Serikali, Mary Lucas, aliwasomea shitaka hilo la jinai namba 413/2014  jana mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Patricia Kisinda.
Alisema kuwa Aprili 16 mwaka huu, wakiwa maeneo ya Levelos, madiwani hao wanadaiwa kumpiga, Mollel kifuani na sehemu mbalimbali za mwili, hivyo kumsababishia maumivu mwilini.
Lucas alisema kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika, hivyo akaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa kwa shauri hilo, huku akiweka wazi kuwa upande wa serikali hauna pingamizi ya dhamana kwa washitakiwa hao.
Madiwani hao walikana shitaka hilo na wako nje kwa dhamana hadi upelelezi utakapokamilika ambapo shauri hilo litarudi mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa Julai 8, mwaka huu.
Katika hatua nyingine, wananchi kadhaa walionekana wakiwa na barua kwa ajili ya kuwadhamini madiwani hao ambao juzi walitangaza kuwa hawako tayari kudhaminiwa ili waende mahabusu kwenye gereza la Kisongo.
Chanzo:Tanzania Daima 

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa