Arusha
Home » » BARUA YA KIOFISI YAMWOKA NAIBU MEYA

BARUA YA KIOFISI YAMWOKA NAIBU MEYA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
NAIBU Meya wa Arusha, Prosper Msofe, amewasilisha mahakamani barua ya kusaini mkataba kati ya Tanzania na Singapore juu ya uandaaji wa mpango wa majiji ya Arusha na Mwanza ili kushawishi apate dhamana.
Hayo yalitokea jijini hapa jana mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Jackson Ndaweka, aliyesikiliza shauri la shambulio la kudhuru mwili linalomkabili Msofe baada ya wakili wa serikali, Diaz Makule kutaka mshitakiwa huyo asipewe dhamana.
Msofe aliileza mahakama hiyo kuwa shitaka linalomkabili lina dhamana, hivyo anaomba apate haki hiyo ili ahudhurie mkutano wa kutiliana saini kati ya nchi hizo kwa mustakabali wa wakazi wa Arusha.
Aliikabidhi barua hiyo kwa hakimu kama uthibitisho, huku akisisitiza kwamba mkutano huo utafanyika kwenye ofisi yake na ujumbe wa watu kutoka Singapore umefika, hivyo asipohudhuria fedha za umma zitapotea.
Wakili Makule alitaka Msofe huyo asipewe dhamana kwa madai kwamba aliendelea kupiga watu hata baada ya kuwa nje kwa dhamana kwenye kesi nyingine iliyokuwa mahakamani hapo wiki iliyopita.
Hakimu Ndaweka aliahirisha kwa saa mbili shauri hilo kisha aliamua kumwachia kwa dhamana Msofe baada ya kuridhika kwamba mashitaka yanayomkabili yana dhamana.
Msofe anatuhumiwa kumpiga mgambo, Wiliam Molel Aprili 16, 2014 na siku hiyo hiyo akiwa Ngarenaro, alimpiga tena mgambo Mary Samwel na kumchania nguo yake.
Shauri limeahirishwa hadi Julai 14, mwaka huu litakapotajwa tena mahakamani hapo.
Chanzo:Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa