Wakuu
wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakizindua kitabu rasmi cha
Muongozo wa Majaji wa Jumuiya hiyo kwenye Mkutano wa 12 wa siku moja wa
Jumuiya hiyo uliofanyika ukumbi wa Kimataifa wa Arusha. Rais
Uhuru Kenyata wa Kenya ambae ndie Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Rais wa
Uganda Yoweri Kaguta Museveni pamoja na Mwenyeji wa Mkutano huo Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Wengine
ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Burundi Bwana Bazombasa, Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyemuwakilisha Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohd Sheni pamoja
na Waziri Mkuu wa Rwanda Bwana Pierre Damieni Habumuryemi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba yaRais wa
Zanzibar Dr. Ali Mohamed Sheni akipokea kitabu wakati wa Mkutano wa
Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mkoani Arusha.
Baadhi
ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania waliohudhuria Mkutano wa 12 wa Wakuu wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Arusha. Wa
mwanzo kutoka kushoto ni Waziri wa Ardhi wa SMZ Mh. Ramadhan Abdulla
Shaaban, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Benard Membe na Waziri
wa Afrika Mashariki Mh. Joh Samuel Sitta.
0 comments:
Post a Comment