Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kesi ya kutakatisha fedha haramu
inayomkabili wakili maarufu jijini hapa, Median Mwale na wenzake watatu,
imechukua sura mpya baada ya upande wa utetezi kudai kesi hiyo
ilifunguliwa kimakosa kabla ya sheria iliyowashtaki kutungwa.
Kutokana na udhaifu huo, wameomba kesi hiyo kuhamishiwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kupata tafsiri ya kisheria.
Aidha wamelalamikia ucheleweshwaji wa makusudi wa
kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo unaofanywa na upande wa Serikali kwa
madai kuwa upelelezi haujakamilika wakati wateja wao wanaendelea kusota
rumande kwa miaka mitatu sasa.
Wakili wa Utetezi, Omary Iddi Omary alisema hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Devota Kamuzora.
Katika kesi hiyo, wakili huyo anasaidiana na
mawakili Mosses Mahuna na Modest Akida huku upande wa Serikali
ukiwakilishwa na Wakili Tumaini Kweka.
Alisema wateja wake, ambao ni Elius Ndenjembi, Don
Bosco Gichana na Bonifasi Mimbwa wanashikiliwa kwa vipindi tofauti kwa
muda wa miaka mitatu sasa.
Alisema kifungu kilichotumika kufungua mashtaka ni
kile kilichofanyiwa mabadiliko Februari 24, 2012 wakati wateja wake
wakiwa mahabusu, jambo alilodai kuwa ni kinyume cha sheria.
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment