Mwandishi Wetu Arusha
Zaidi
ya wafugaji 300 wa Kuku na mifugo mbalimbali na wafanyabishara wa
maduka ya madawa ya kilimo na mifugo wamepatiwa mafunzo ya utumiaji dawa
mbalimbali za kutibu mifugo ya aina mbalimbali na virutubisho
mbalimbali vinavyotolewa na kampuni ya BYTRADE (T) LTD ilikukwepa
magonjwa ya mafuwa na aina nyingine za magonjwa na virutubisha vya
mifugo.
Akizungumza
katika semina ya kuwajengea uwezo wafugaji na wauza dawa za mifugo mkuu
wa idara ya wanyama wa kampuni ya Bytrade Dkt Omary Magoma alisema kuwa
aina mbalimbali za mifugo zimekuwa zikisumbuliwa na maradhi mbalimbali
na zinahitaji dawa za kuyatibu maradhi yao ili kuweza kupata suluhu.
Magoma
pia akawataka wafugaji pindi wanapoona wanyama wao wana hali dhaifu
kuacha kuwapa dawa bila ya kugundua ugonjwa huku pia wakiendelea
kuteketea na kuwashauri kutumia bidhaa za kampuni hiyo kwani ndio suluhu
ya matatizo ya magonjwa na virutubisho ya wanyama na mimea.
“Kwa
mfano dawa hii ya GUT-O-CID ni dawa ya kudhibiti kwa ufanisi bacteria
waenezao magonjwa sumbufu kama salmonella,E.coli pia inadhibiti
uzalishwaji wa gesi ya ammonia inayosababishwa harufu kali bandani
ambayo ni chazo cha mafua makali kwa wanyama aina ya Kuku na
Nguruwe”alisema Dkt Magoma.
Dawa
hiyo ambayo huchanganywa kwenye chakula ukilinda chakula hicho dhidi ya
maambukizi ya bacteria na fangasi na pia huongeza ladha ya chakula
akabainisha kuwa kwa sasa wameingiza dawa aina kumi na moja sokoni na
zinapatkana kwenye maduka mbalimbali ya madawa ya mifugo humu nchini.
Dkt
Magoma alizitaja baadhi ya dawa hizo kuwa ni suluhu ya maradhi
yanayowaandama wanyama wafugwao kwa mfano dawa hii ya Mult-Aminovet ina
aina zote za vitamin na amino acid pia madini kuweza kufidia mapungufu
katika vyakula vya wanyama na kuboresha kiwango cha utagaji na ubora wa
mayai.
Pia
inaongeza matokeo bora kwa Ng’ombe wa maziwa na hutumika kuondoa stress
wakati wa matibabu,chanjo,joto kali na usafirishaji kwa kuku huku pia
akiitaja dawa aina ya Enziver kuwa inaboresha uyeyushwaji na unyonywaji
wa chakula mwilini mwa wanyama na pia huraisisha ukuaji na ongezeko
kubwa kwa Kuku na Nguruwe.
Huku
akiwata watanzania hususani wafugaji kuanza kutumia dawa za kampuni
hiyo kwani ndiyo suluhu ya kupata mifugo bora kwani dawa wanazouza zipo
kwenye viwango vilivyo bora.
0 comments:
Post a Comment