Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
TAASISI za elimu nchini zimeshauriwa kuongeza mitaala ya
ujasirimali shuleni ili kuwawezesha wanafunzi wanaomaliza masomo katika
ngazi zote kuanzia shule za msingi na sekondari kuwa na uwezo wa
kujiajiri bila kutegemea ajira za serikali.
Wito huo ulitolewa mjini hapa jana katika Shule ya Sekondari Ganako
na mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Babson kilichopo Jimbo la Boston,
Marekani, Profesa Dennis Hanno wakati akikabidhi vyeti vya uhitimu kwa
wanafunzi 119 kutoka shule tatu za sekondari mjini Karatu ambao
walipata mafunzo ya ujasiriamali.
Mafunzo hayo yalitolewa na wanafunzi 10 wa Chuo Kikuu cha Babson kwa
usimamizi wa mkufunzi huyo ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo kama hayo
ambayo wameyatoa Rwanda, Uganda na Ghana.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment