Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgomo wa mabasi yanayofanya safari zake kati ya
Moshi na Arusha, jana ulitikisa miji hiyo kwa saa nane mfululizo, huku
baadhi ya daladala za katikati ya Mji wa Moshi nazo zikishiriki mgomo
huo.
Polisi wa kutuliza ghasia (FFU), wakiwa na magari
sita, huku wamejihami kwa silaha yakiwamo mabomu ya machozi, walionekana
wakizunguka mitaani na kupeperusha bendera nyekundu.
Kituo Kikuu cha Mabasi ya Moshi-Arusha na miji
mingine, jana saa 2:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana, kilizingirwa na
polisi na hakuna basi lililoingia kituoni wala kutoka.
Mbali na kituo hicho kuwekewa ulinzi mkali, FFU,
wakipeperusha bendera nyekundu, waliweka kambi Kituo Kikuu cha Polisi,
Moshi tayari kudhibiti vurugu kama zingetokea.
Kutokana na mgomo huo, baadhi ya abiria kutoka
maeneo mbalimbali walilazimika kutembea kwa miguu kwenda kwenye shughuli
zao mbalimbali.
Mgomo huo ulianza saa 12:00 asubuhi ukishirikisha
mabasi mengi kabla ya kuanza kupungua nguvu saa 3:00 asubuhi baada ya
baadhi ya wamiliki kulegeza msimamo.
Hata hivyo, ahueni hiyo ilikuwa ya muda mfupi tu, kwani saa moja baadaye mabasi karibu yote yaliingia katika mgomo.
Wakati hali ikiwa hivyo, madereva wa pikipiki
maarufu kama ‘Bodaboda’ walinufaika na mgomo huo kwani watu walilazimika
kutumia vyombo hivyo vya usafiri.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji Kilimanjaro
na Arusha (Akiboa), Hussein Mrindoko alisema jana kuwa sababu ya mgomo
huo ni faini kubwa wanazotozwa na askari wa Usalama Barabarani.
Chanzo ;Mwananchi
Chanzo ;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment