Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
DIWANI
wa Levelosi, Ephata Nanyaro (CHADEMA), ametoa msaada wa unga, mahindi
na sukari kwenye Shule ya Msingi Levelosi ili kuwawezesha wanafunzi
kupata uji nyakati za mchana baada ya serikali kushindwa kuwapatia
chakula wawapo shuleni.
Nanyaro alitoa msaada wa sukari kilo 105 na unga wa mahindi kilo 220
juzi na kukabidhiwa kwa mwalimu wa chakula, Frida Malya, mbele ya
Mwalimu Mkuu, Elisante Kaaya, walimu wengine na wanafunzi wa shule
hiyo.
Alisema ataendelea na utaratibu wa kupeleka msaada kama huo ili
kuhakikisha wanafunzi wanapata uji kwa kipindi chote cha mwaka, jambo
alilosema litasaidia kuwapunguzia wanafunzi njaa.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment