Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Hatimaye Halmashauri ya Jiji la Arusha imeanza kubomoa nyumba
zaidi ya 300 baada ya malumbano ya kisheria mahakamani, yaliyochukua
muda mrefu.
Ubomoaji ulianza asubuhi chini ya usimamizi wa
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Elphas
Mollel, wakuu wa idara mbalimbali za halmashauri ya jiji, huku polisi
wakiimarisha ulinzi.
Tofauti na ilivyodhaniwa kungetokea upinzani mkali
kutoka kwa wapangaji, hali ilikuwa ya utulivu, huku wapangaji
wakikusanya vitu vyao ili visiharibiwe na tingatinga zilizokuwa
zikibomoa nyumba hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela alisema
nyumba hizo zimejengwa miaka mingi iliyopita na kupuuza kauli za
wapangaji kuwa wana haki ya kumilikishwa nyumba hizo kwa kuwa wameishi
kwa muda mrefu.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Elphas Mollel
alisema Kata ya Levolosi eneo la Samunge jumla ya nyumba 56, Kata ya
Kaloleni nyumba 198 na Kata ya Themi ni 84 zinabomolewa, ili kupisha
uwekezaji mkubwa na wa kisasa..
Hata hivyo, alisema nyumba mbili hazitabomolewa
kutokana na moja kuwa na utata wa kisheria ambayo mmiliki anadai kuuziwa
na Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), wakati nyingine alisema Rais
wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi aliitoa kwa mama mkongwe.
Chanzo;mwananchi
Chanzo;mwananchi
0 comments:
Post a Comment