Home » » TRA yatangaza vita na wataohamasisha mgomo

TRA yatangaza vita na wataohamasisha mgomo


index
Na Gladness Mushi, Arusha
MAMLAKA ya mapato TRA hapa nchini imetangaza vita kubwa kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa ambao wanashinikiza mgomo wa kufunga biashara kwenye maduka mbalimbali hapa nchini kwa visingizio vya kutotambua matumizi ya mashine za kulipia kodi
Aidha hatua hiyo inakuja wakati wafanyabiashara katika mikoa mbalimbali hapa nchini kufunga maduka na kisha kushinikiza kwa wenzao wasitoe huduma kwa ajili ya kupinga matumizi ya mashine hizo
Akitangaza rasmi vita hiyo ambayo itafanyika katika mikoa yote hapa nchini kaimu  Kamishna mkuu wa mamlaka hiyo Rishedi Bade alisema kuwa serikali kamwe haitaweza kuwafumbia macho wadanganyifu wa biashara ya aina yoyote ile
Alisema kuwa kwa wafanyabiashara wa aina yoyote ile atakayekamatwa kuwa anashinikiza mgomo basi wataweza kuchukuliwa sheria mbalimbali ambazo zitawagarimu kwa kiwango kikubwa sana
Pia aliwataka wafanyabiashara nao kutoingia kwenye mgomo ambao hauwahusu kwani wanajitengenezea harasa zao wenyewe wakati wanaohitajika kutumia mashine hizo za kielekroniki wamebainishwa kwenye sheri
“TRA tunashangaa sana kuona kuwa wafanyabiashara wasiohusika wanafunga biashara wakati wanaohusika ni wengine na kwa hali hiyo tunatangaa vita sasa na wale ambao wanahamasisha mgomo”aliongeza Bade
Wakati huo huo pia alisema kuwa watakaokamatwa wakiwa wanahasisha mgomo huo hatua watakazochukuliwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani lakini pia hata kuweza kuwafutia leseni zao za biashara
Katika hatua nyingine alisema kuwa matumizi ya mashine hizo ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa la Tanzania kwani zinaweka na kuanisha wazi juu ya mapato halisi ya mfanyabiashara

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa