JESHI la Polisi mkoani Arusha, linamshikilia mahabusu wa Gereza la
Kisongo, kwa kosa la kumuua kwa kumpiga jiwe kichwani askari polisi
mwenye namba 5264 Sabato. Mahabusu huyo, Njoke Ole Kibhip (34), alitenda
kosa hilo juzi katika eneo la uwanja wa ndege Arusha, wakati akitolewa
mahakamani kurudishwa mahabusu.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Lebaratus Sabas, alisema askari huyo na mtuhumiwa walitoka katika Mahakama ya Wilaya ya Longido wakiwa wanaongozana kama ilivyokawaida.
“Tumempoteza askari wetu aliyeuawa kwa kupigwa jiwe kichwani na mahabusu niliyemtaja hapo juu, inaonekana mtuhumiwa alikuwa anataka kutoroka.
“Walitoka wote katika Mahakama ya Wilaya ya Longido, wakirudi gerezani, sasa wakati wamefika uwanja wa ndege yule mahabusu aliomba afunguliwe pingu ili ajisaidie haja ndogo… inaonekana alikuwa anatafuta njia ya kutenda uhalifu.
“Baada ya kufunguliwa alitumia mwanya huo kumvizia askari na kumrushia jiwe ambalo lilimpiga vibaya kichwani.
Alisema tukio hilo, lilitokea saa 5 asubuhi na mwili wa askari Sabato umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru), kusubiri taratibu za kuusafirisha kwenda nyumbani kwao wilayani Ukerewe.
Alisema uchunguzi wa tukio hilo, unaendelea na pindi utakapokamilika mahabusu huyo atafikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili.
Chanzo;Mtanzania

0 comments:
Post a Comment