Home » » MWIGULU NCHEMBA AZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA MADIWANI JIJINI ARUSHA LEO

MWIGULU NCHEMBA AZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA MADIWANI JIJINI ARUSHA LEO


Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara Mh;Mwigulu Nchemba ameshawasili Jijini Arusha Mchana huu akitokea Kiteto na Babati kwa ajili ya Uzinduzi wa Kampeni za Udiwani zinazoendelea nchi nzima,Chaguzi hizi ni ndogo kwa ajili ya kujaza nafasi za Madiwani waliojiuzulu na wengine kufariki. Naibu Katibu Mkuu CCM Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameambatana na Mgombea wa Udiwani Kata ya Sombetini WIlaya ya Arusha ndugu David,Hapa akiwa kwenye maandamano kutokea Ofisi za chama hapa Sombetini kuelekea Viwanja vya Mkutano,Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha.
Mh:mwigulu Nchemba akipata mapokezi mazito kutoka kwa maelfu ya wananchi waliomiminika Viwanja hivi vya Soko la Mbauda kwaajili ya Mkutano wa hadhara wa kampeni za Udiwani. Mapokezi yanaendelea hapa Soko la Mbauda kwa ajili ya kuanza mkutano wa hadhara.
Sehemu ya Mamia ya Wananchi wakiwa tayari kusikiliza Mkutano huu wa hadhara kwaajili ya Kampeni za Udiwani kata ya Sombetini jijini Arusha. Wananchi wanaendela kumiminika kwenye viwanja hivi vya soko la Mbauda kwenye Mkutano wa Hadhara wa CCM kumnadi mgombea wa CCM kwenye Kinyang'anyiro cha Udiwani.
Kwa hisani ya Jiachie Blog

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa