Hali
ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), bado haijatulia
tangu Kamati Kuu ilipomvua nyadhifa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama
hicho, Bara, Zitto Kabwe pamoja na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk.
Kitila Mkumbo.
Hali imeonekana kuwa si shwari baada ya jana, Baraza la Uongozi mkoani Arusha, kumvua Uenyekiti wa Wilaya ya Monduli, Mchungaji Amani Silanga Mollel, baada ya kuitisha kikao cha kumtetea Zitto.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Chadema Mkoa Arusha na Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, alisema Mollel amevuliwa Uenyekiti Ijumaa iliyopita baada ya kubainika kuwa alitoa tamko batili, akitumia wadhifa wa mwenyekiti wa wilaya, bila ridhaa ya kamati tendaji na huku akidanganya kuwa ni tamko kwa niaba ya wilaya hiyo.
Golugwa alisema hatua ya Mollel kumtetea Zitto anavunja kanuni za chama kwa mujibu wa katiba ya chama toleo la mwaka 2006 ya Kanuni za uendeshaji kazi za chama, sura ya kumi, Ibara ya 10 (x).
“Kiongozi asitoe tuhuma juu ya viongozi wenzake, pasipo kupitia vikao halali na kuzingatia taratibu na ngazi zilizoelezwa kwenye kanuni za chama,” alisema Golugwa.
Alisema Mollel alitoa tuhuma za uzushi, uongo na upotoshaji na kutaka kuaminisha jamii kuwa Chadema ina makundi ya Chadema Asili na Chadema Family, kitu ambacho ni upotoshaji wa hatari kwa ustawi na umoja wa chama na kinyume na kanuni za uendeshaji kazi za chama, sura ya kumi, Ibara ya 10 (VII).
Golugwa alisema kutokana na makosa hayo, Chama kilimtaka aonyeshe Chadema Asili ni kina nani na Chadema family ni kina nani, na alishindwa kutoa maelezo yoyote ya maana na kufikia hatua ya kutaka kuvuruga kikao kwa kuleta vijana wahuni 17 ndani ya kikao, ambao wengi walijulikana kuwa siyo wanachama wa chama hicho.
Alisema Mollel alikiri kuwapo kambi ya Zitto na hakuna wa kumfanya kitu, maana ni mjumbe wa baraza kuu la chama.
“Maneno haya yalidhihirisha kuwa Mchungaji Silanga anashiriki mpango wa kuunda makundi yasiyo na tija, ndani ya chama na hivyo kuwa kinyume katiba ya chama inavyotaka,” alisema Golugwa.
Alisema kutokana na hali hiyo, Baraza la uongozi la Mkoa lililoketi Novemba 29, limeridhia kuwa amevunja kanuni za maadili ya chama, sura ya 10 Ibara ya (VII) hadi (XII) na hivyo kupendekeza kumvua nafasi yake.
Golugwa alisema uchunguzi zaidi dhidi yake unaendelea, ili kufikia maamuzi makubwa zaidi ya tuhuma nyingi kwa mujibu wa kanuni za hatua za kinidhamu.
MWANZA WAKOROGANA
Wakati hali ikiwa hivyo Kaskazini, matawi 189 ya Chadema katika Mkoa wa Mwanza yametoa tamko kuwa kumeibuka ombwe kubwa kwa baadhi ya viongozi wa juu kujitwalia mamlaka ya chama kinyume cha Katiba ya chama.
Mwenyekiti wa Vijana Kanda ya Ziwa Magharibi, Robert Gwanchele, katika taarifa yake jana kwa vyombo vya habari alisema sababu zilizotolewa na Kamati Kuu (CC) ya Chadema ya kumvua nyadhifa Zitto na Dk. Mkumbo hazikubaliki.
Alisema maamuzi ya CC yameonyesha woga wa demokrasia kwa viongozi wa Chadema kuikwepa demokrasia kwa kisingizio cha kusaliti na uhaini ndani ya chama.
Alisema sababu za kuandamwa kwa Zitto na Dk. Mkumbo ni kwa sababu wanahoji mapato na matumizi ya chama zikiwamo fedha zinazotolewa na serikali kama ruzuku pamoja na harambee za M4C Mwanza, Arusha na Dar es saalam.
CHADEMA WAKANUSHA
Hata hivyo, Viongozi wa Chadema wilaya ya Ilemela wamesema Gwanchele aliyetoa taarifa hiyo siyo kiongozi ndani ya chama na kwamba amefanya hivyo kwa kutumiwa na watu ambao ni wapinzani wa Chadema.
Mwenyekiti wa Vijana Wilaya ya Ilemela, Damas Kimenyi na Katibu Froling Rwela, wakizungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti walisema Gwanchele siyo kiongozi ndani ya chama na hata cheo cha Mwenyekiti wa Vijana Kanda ya Ziwa Magharibu hakipo ndani ya chama.
Walisema Gwanchele alikuwa Katibu wa Chadema kata ya Nyamanolo lakini alivuliwa wadhifa huo mwaka 2011 baada ya kubainika alikuwa akitumiwa kukihujumu chama na hivyo kubakia kuwa mwanachama wa kawaida.
“Ndani ya chama Mwenyekiti wa Kanda ya Ziwa Magharibi ambaye ni Peter Mekele, Katibu ni Renatus Bujiko, kwa hiyo cheo cha Mwenyekiti wa Vijana wa Kanda ya Ziwa Magharibi hakipo katika Chadema, taarifa aliyoitoa anatumiwa na CCM,” walisema.
Viongozi hao walisema kuwa Chadema wilaya ya Ilemela na mkoa wa Mwanza kwa ujumla ilishatoa taarifa ya kuunga mkono uamuzi uliotolewa na Kamati Kuu ya kuwavua nyadhifa Zitto na Dk. Mkumbo.
Zitto na Dk. Mkumbo walivuliwa nyadhifa zao wiki iliyopita kwa kile kilichodaiwa wamekisaliti chama kwa kuandaa 'Waraka wa Mabadiliko mwaka 2013' ambao ulilenga kuandaa mtandao wa ushindi kwenye uchaguzi wa ndani ya chama mwakani.
Baada ya uamuzi huo wa CC, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Said Arfi, alijiuzulu wadhifa huo. Imeandikwa na Thobias Mwanakatwe; Dar na Cynthia Mwilolezi, Arusha

CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment