Arusha.Serikali inakusudia kupitia upya sheria
na kanuni za kodi pamoja na mazingira yote ya biashara katika sekta ya
utalii kwa lengo la kuwaondolea kero wadau wa sekta hiyo ili kuongeza
mchango wake katika pato la taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamisi
Kaghasheki alisema ili kufikia lengo hilo, Serikali itakuwa ikifanya
vikao vya kila robo mwaka na wadau wa sekta hiyo kujadili changamoto
zinazowakabili na njia za kuyakabili.
Akizungumza juzi jijini Arusha wakati wa chakula
cha jioni kilichoandaliwa na Chama Cha Wafanyabiashara wa Utalii nchini
(Tato), Balozi Kaghasheki alisema ni lengo la Serikali kuongeza idadi ya
watalii kutoka milioni moja mwaka huu mpaka kufikia watalii 1.5 milioni
kufikia mwakani.
“Tanzania ni nchi ya pili kwa kwa na vivutio vingi vya utalii duniani baada ya nchi ya Brazil,” alisema Kaghashekil.
Aliongeza: “Lakini ni ya 114 kwa utoaji huduma za
kitalii. Lazima tujiulize nini kifanyike ili tungoze katika sekta hiyo
muhimu,” alisema Kaghasheki.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment