Waliopinga maamuzi waomba radhi
Mkuu Kanda ya Kaskazini,Amani Golugwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Japhet Lusingu, alisema polisi inaendelea kuwahoji watu hao, ili kubaini ukweli wa tukio hilo.
Alisema uchunguzi uliofanywa na polisi kwa kushirikiana na Idara ya Zimamoto, imegundua kuwa Ofisi za Chadema zinalindwa na walinzi wa chama hicho na kuwa mlinzi Bahati aliingia kazini saa 12:00 jioni na kutoka Desemba 3 saa 12:00 asubuhi pia Katibu Muhtasi Mwasha ambaye alikuwa akiingiza kazini saa 1:30 asubuhi kila siku, lakini siku ya tukio aliingia saa 4:00 asubuhi.
Wakati huo huo viongozi wanne wa Chadema Mkoa wa Tanga, wamedaiwa kukiri kuhusishwa katika mtandao wa kukivuruga na wameomba kusamehewa wakidai kwamba walidanganywa.
Viongozi hao ambao waliwahi kutoa tamko la kupinga maamuzi ya Kamati Kuu ya Chadema kwa kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo na Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, waliomba radhi mbele ya katibu Mkuu Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Golugwa alisema viongozi hao Tanga wameomba kusamehewa.
Alisema walikiri kuwa walikuwamo katika mtandao ujulikanao (MK1-50) na kwamba waliamua kupinga kwenye vyombo vya habari maamuzi ya Kamati Kuu kutokana na kudanganywa.
“Miongoni mwa majukumu yaliyonileta hapa Tanga ni kuwashughulikia hawa viongozi waliotoa matamko ya kupinga maamuzi ya chombo halali cha Kamati Kuu, lakini wameomba msamaha na kukiri kuwa walidanganywa,”alisema na kuongeza kuwa wamesamehewa, ingawa wataendelea kufuatiliwa nyendo zao.
Katibu huyo alisisitiza kuwa kinachoendelea hivi sasa ndani ya Chadema ni kutumbua majipu yaliyokuwa yakikisumbua na kwamba hakitarejea nyuma bali kitahakikisha kinasafishika.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment