Wilaya ya Arusha Vijijini imefanikiwa kukusanya kiasi cha Milioni 682 sawa na asilimia 31.8 kutoka katika vyanzo vyake vya mapato ingawaje kwa kipindi cha mwaka 2013,2014 wanatarajai kukusanya kiasi cha zaidi ya bilioni mbili sanjari na kuibua vyanzo vya mapato ambavyo vitaimarisha zaidi uchumi wa wananchi wake.
Hayo yamelezwa mapema jana na Kaimu mweka wa Halmashauri hiyo bw Munguabela Kakulima wakati akielezea Vyanzo vya mapato ambavyo vitakwenda sanjari na mpango wa matokeo makubwa (Big Result Now)kwenye wilaya hiyo
Kakulima alidai kuwa kupatikana kwa fedha hizo kunatokana na jitihada mbalimbali ambazo zinafanywa na idara yake ambapo ndipo zilipochangia mafanikio hayo.
Aidha alidai mpaka mwaka wa fedha wa sasa uweze kuisha wanatarajia kuvuka hata lengo ambalo walikuwa wameliweka na hivyo kukusanya fedha nyingi zaidi hali ambayo itachangia shuguli mbalimbali za maendeleo kuweza kufanyika kwa haraka.
Mbali na hayo alidai kuwa kwa sasa wanamikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa wanaweka uwezekano wa kubaini vyanzo vipya vya mapato ambavyo navyo vitaweza kuweka halmashauri hiyo kwenye kiwango cha juu sana.
Mkakati mwingine ambao nao aliweza kuutaja ni pamoja na kuweza kuwapa wananchi elimu ya kuweza kulinda vyanzo vya mapato lakini kuweza kuonesha umoja baina ya watendaji wa halmashauri hiyo ili kuweza kuharakisha shuguli mbalimbali za ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
Awali alisema kuwa pamoja na mikakati na jitiada ambazo zinafanywa na idara ya fedha katika Halmashauri hiyo zipo changamoto ambazo nazo zinachangia kukwamisha malengo mbalimbali ya ukusanyaji wa mapato kutoka katika vyanzo.
Kakulima alidai kuwa changamoto hizo ni pamoja na baadhi ya wanasiasa kuingilia shuguli pamoja na vyanzo vya mapato hali ambayo wakati mwingine inasababisha waone kuwa halmashauri hiyo inachangia sana kuwadidimiza.
Naye mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema kuwa ili matokeo ya haraka yaweze kuja katika Halmashauri hiyo vyanzo vya mapato vinatakiwa kulindwa lakini nao watendaji wa idara ya fedha wanatakiwa kufuata wajibu wao wa kulinda na kuitetea halmashauri hiyo.
Chanzo;Fullshangwe
0 comments:
Post a Comment