Arusha
Home » » Jeshi la polisi Jijini arusha lakitaka Chama cha Chadema kutofanya shughuli zozote kwenye viwanja vya Soweto

Jeshi la polisi Jijini arusha lakitaka Chama cha Chadema kutofanya shughuli zozote kwenye viwanja vya Soweto

Mahmoud Ahmad,Arusha

Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo (CHADEMA) kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo huku mabomu yakirindima uwanjani hapo.

Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani hapa Liberatus Sabas alisema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu upelelezi. Kamanda Sabas alisema kuwa kwa hiyo jeshi hilo limewataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.

Hali kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangia juzi kwa wafuasi wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza tukio la bomu la kurushwa kwa mkono lililotokea uwanjani hapo juzi.

Hata hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikuwa wamukusanyana kwenye uwanja huo hali iliyoendelea kuleta mvutano kati ya viongozi wa jeshi la polisi na wafuasi hao baada ya kukaidi amri ya jeshi hilo mabomu yalirindima uwanjani hapo.

Baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho walikuwepo uwanjani hapo akiwemo mbunge wa jimbo la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje na wabunge mbali mbali wa chama hicho walikuwa kwenye kikao cha bunge kinachoendelea hali hiyo imeliweka jiji hili kusimama shughuli zake kutokana na mabomu hayo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa