Arusha
Home » » BREAKING NUUZ! MABOMU YARINDIMA ARUSHA KUTAWANYA WANAODAIWA WAFUASI WA CHADEMA, SUGU ANUSURIKA KUFA APATA AJALI AKIELEKEA ARUSHA

BREAKING NUUZ! MABOMU YARINDIMA ARUSHA KUTAWANYA WANAODAIWA WAFUASI WA CHADEMA, SUGU ANUSURIKA KUFA APATA AJALI AKIELEKEA ARUSHA


Habari zilizotufikia hivi punde chumba cha habari cha mtandao huu, zinasema kuwa Hali si shwari katika jiji la Arusha, ambapo hadi muda huu bado mabomu ya machozi yanaendelea kurindima baada ya Askari Polisi kuanza zoezi hilo kwa ajili ya kuwatawanya watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa CHADEMA, waliokusanyika katika viwanja vya Soweto wa ajili ya maombolezo ya watu waliofariki katika tukio la mlipuko wa bomu lililotokea mwishini mwa wiki iliyopita katika mkutano wa Chadema.

Aidha imeelezwa kuwa awali watu hao walizuiliwa kukusanyika eneo hilo na baadaye viongozi wa chadema walipofika eneo hilo walianza kuwahutubia wananchi waliokusanyika eneo hilo jambo ambalo lilizuiliwa huku vijana wakiimba nyimzo za maombolezo na za siasa, jambo lililowafanya askari kuchukua jukumu la kuwatawanya kwa mabomu ya machozi.

WAKATI HUO HUO:- habari zinaendelea kusema kuwa Mbunge wa Mbeya mjini JOSEPH MBILINYI Mr. ii, SUGU, amenusurika kufa baada ya kupata ajali eneo la Katesh Wilaya ya AHanang mkoa Manyara  wakati akiwa njiani kuelekea jijini ARUSHA.

Polisi Mkoa wa Arusha inawashikilia baadhi ya Viongozi wa CHADEMA, Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu na viongozi wengine kwa kuitisha mkutano usiokuwa halali ili kuondoa uvumi wa kuwa mbunge amefariki Dunia.
 
CHANZO :  SUFIANI MAFOTO BLOG

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa