Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini TCAA
imeanza kufanya uchunguzi wa kitaalamu kubaini chanzo cha ajali ya ndege
iliyotokea mkoani Arusha jana na kusababisha kifo cha rubani wake.
Ndege hiyo ndogo yenye uwezo wa kubeba kati ya
watu 4 hadi sita ilianguka juzi jioni majira ya saa 12:45 wakati ikajaribu
kutua kwenye uwanja wa ndege wa arusha.
Aliyefariki katika ajali hiyo ametambuliwa kuwa
ni mfanya biashara maarufu wa wa mjini moshi Joseph Malya
almaarufu kwa jina la Bob Sambeke.
Meneja wa mamalaka ya viwanja vya ndege
mkoani Arusha Bwana Aswile Kamendu amewaambia
waandishi wa habari kuwa ofisi yake inasubiri mtaalamu
kutoka wizara ya uchukuzi ili kuendelea na uchunguzi wa kina
uliosababisha ajali hiyo ya ndege.
Taarifa za awali zilizowakariri mashuhuda zinadokeza
kuwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano kisha ,kuanguka kando ya mti mkubwa
eneo la magereza mita 200 kutoka barabara ya kurukia ndege katika
uwanja huo.
Mapema jana jioni ndugu wa marehemu Mallya
waliokuwa katika harakati za kusafirisha mwili wake kutoka hospitali ya
mkoa wa arusha mount Meru hadi mjini moshi kusubiri taratibu za maziko.
Ajali
za ndege katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro zimekuwa zikiripotiwa kuongezeka
ambapo jumla ya ndege 4 na helkopita moja zimeanguka katika kipindi cha miaka
saba iliyopita na kusababisha vifo,majeruhi na uharibifu mkubwa wa mali
0 comments:
Post a Comment