Na
Charles Ngereza
Watu
wawili kutoka jamii ya Waarusha wilayani Arumeru wamejeruhiwa vibaya kwa
kukatwa katwa kwa sime na kundi la morani wa Kimasai kutoka wilayani Longido
katika mzozo unaoendelea wa kugombea eneo la malisho kati ya jamii hizo.
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa lilitokea juzi eneo la Ilkidotu katika mpaka wa wilaya za Longido na Arumeru baada ya watu hao kuingiza mifugo katika Wilaya ya Longido kupata malisho.
Akizunguzungumza kwa taabu hosptalini jana, mmoja wa majeruhi Miruti Narumusha, alisema walivamiwa na kundi la morani zaidi ya 50 na kuwashambulia kiasi cha kupoteza fahamu na baadaye kuokolewa na ndugu zao na kupelekwa hospitalini hapo.
“Tulikuwa tunachunga kundi la ng'ombe kama mia tatu na hawa Wamasai walituvizia kwani tulishangaa tumezingirwa na tukazidiwa nguvu, walitupiga na nadhani waliondoka wakijua tumekufa,” alisema Narumusha.
Alisema mpaka sasa hafahamu mahali walipo ng’ombe wake baada ya tukio hilo ambalo anasema lilikuwa baya sana kuwahi kumtokea katika maisha yake.
“Sisi Waarusha kwa kweli hatutaki kupigana, tuliutii wito wa Mkuu wa Mkoa wa kurudi nyuma na kuacha mapigano na mgogoro ulitatuliwa kwa njia ya amani, lakini namna wanavyofanya ndugu zetu Wamasai inazidi kuleta hatari,” alisema Narumusha.
Majeruhi mwingine, Seuri Nyangusi, alieleza kuwa siku ya tukio aliwaona morani wa Kimasai wakiwa wamezingira eneo walilokuwa wakichunga mifugo yao na baadaye wakashambuliwa.
“Jana ndiyo nimeanza kupata fahamu, lakini nakumbuka tu kwamba walitutegea tulipofika eneo la bonde ndipo wakaanza kutushambulia, nilipoteza fahamu na baada ya siku moja nimejikuta hapa,” alisema Nyangusi.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas, alisema tukio hilo ni la kihalifu.
Kamanda Sabas alisema polisi inawasaka wahusika ili wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.
“Hawa ni watu wachache ambao naamini tutawakamata, tulikwisha rejesha amani katika eneo hilo na viongozi wa jamii hizo wanaendelea na vikao vya kumaliza tatizo, hawa wanaoanzisha vurugu tutawashughukia kisheria,” alisema Kamanda Sabaa.
NIPASHE lilishuhudia magari mawili ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yakiwa yamejaa askari wenye silaha wakifanya doria katika eneo la Engikaret na Longido jana.
Kufuatia vurugu hizo, soko la Oldonyosambu ambalo hufanyika kila siku ya Jumamosi na kuhudhuriwa na wafanyabiashara wengi wa Wilaya ya Longido, juzi lilonekana kudorora kufuatia hofu ya kutokea vurugu.
“Hali ya soko ilikuwa mbaya hata wafanyabiashara kutoka maeneo mengine hawakufika kwa kuwa mapigano yalianzia katika hili soko,” alisema mfanyabiashara, Anthony Mbise.
Alisema siku ya tukio, wafanyabiashara kutoka Longido, Kiseriana na Engarenaibor, walipoteza mifugo yao na kupata hasara.
“Sijui itakuwaje kwani Wamasai walipigwa na wengi walipoteza pesa na mifugo waliyoleta kuuza katika soko hili, sijui kama watarudia kufanya biashara hapa,” alisema Mbise.
Tukio hilo linatokea wakati Serikali ya Mkoa wa Arusha ikiwa imetangaza kumaliza mgogoro huo ambao umesabisha maboma 12 yenye nyumba 80 kuchomwa moto na watu zaidi ya 400 kukosa makazi na wengine 20 kujeruhiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alipoulizwa kwa njia ya simu jana, alisisitiza kuwa hakuna vita katika eneo hilo na vyombo vya usalama vinaendelea kungalia hali ya usalama.

Chanzo:
Nipashe
0 comments:
Post a Comment