Arusha
Home » » WATANZANIA WAMETAKIWA KUVIPENDA VIVUTIO VYA UTALII NA KUJENGA MAZOEA YA KUVITEMBELEA.

WATANZANIA WAMETAKIWA KUVIPENDA VIVUTIO VYA UTALII NA KUJENGA MAZOEA YA KUVITEMBELEA.


Mahmoud Ahmad  Arusha.
Watanzania wametakiwa kuvipenda vivutio vya utalii na kujenga mazoea ya kuvitembelea kwani ni urithi  waliojaaliwa na Mwenyezi Mungu na kuvithamini sanjari na utunzaji wa vivutio hivyo kwani ni njia ya kuwapatia maendeleo na ajira itakayolipaitia taifa letu maendeleo endelevu kwani sekta hiyo inakuwa kwa kasi siku hadi siku.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi (pichani) wakati akiwasilisha mada kwenye kongamano la kimataifa la utalii (UNWTO) linaloendelea mjini Arusha  na kutanabaisha kuwa sekta hiyo imekuwa na changamoto nyingi katika ukuaji wake ikiwemo njia za kuitangaza kimataifa na hapa nchini.
Kijazi amesema kuwa ili kuwa na uchumi endelevu kwenye sekta ya utalii tunahitaji kufuta sheria ya taifa ya ukuaji wa uchumi ya mwaka 2004, kwa kuwekeza kwenye sekta hiyo ili kuweza kutupatia kipato cha kujenga taifa na wananchi waweze kupata faida ya kiuchumi kutokana na rasilimali zao.
Aidha amesema ili kuwa na nguvu ya kuyafanya haya yote tunahitaji kuunganisha nguvu kwenye mipango endelevu ya kuutangaza utalii wa ndani na nje ya nchi zetu, na kutolea mfano wa nchi zilizopiga hatua kamaAfrika kusini na Botswana.
Kijazi amesema kuwa mazingira ya vivutio vyetu yanavutia kwa watalii na kuwa ni sehemu ya kuendesha uchumi wa nchi yetu, hivyo tuna kila sababu ya kujivunia kuwa watanzania na kuendelea kuvitangaza vivutio hivyo popote ulimwenguni bila ya kusubiri kuwa kazi hiyo ni ya serikali pekee.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa