Home » » WAKULIMA WA MTAMA WAILILIA SERIKALI

WAKULIMA WA MTAMA WAILILIA SERIKALI

Na Mary Mwita, Arusha
SERIKALI imeombwa kuwasaidia wakulima wa zao la mtama, ili waweze kupata soko la uhakika la kuuza mazao yao. Akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao la uwele na mtama mjini Arusha juzi, Mratibu wa taasisi ya HOPE Afrika Mashariki, Dk. Frida Mgonja, alisema zao la mtama halina soko la uhakika.

“Zao hili halina soko la uhakika, licha ya umuhimu wake, wadau wa kilimo wanatakiwa kushirikiana na Serikali, kuhakikisha wakulima wanaozalisha mtama wanapata soko la uhakika.

“Tayari tumeweza kuhamasisha wakulima waendelee kulima zao la mtama wa kisasa, ambapo wakulima wengi wameitikia wito wa kulima zao hilo,” alisema.

Naye, Mratibu wa mradi huo Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Dk. Mary Mgonja alisema, mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Dk. Mgonja alisema, kwa sasa Tanzania inatajwa kuwa nchi bora katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini, kwa kuzalisha mtama bora.

Aliwataka wakulima kuzalisha mazao yao katika hali ya usafi, kwa kuzingatia ukweli kuwa mtama unatumika katika kutengenezea vinywaji pamoja na chakula.

Mkutano huo unakutanisha wadau mbalimbali wa kilimo cha mtama na uwele, kutoka Wilaya za Singida, Kondoa, Kishapu, Arusha na wadau wengine kutoka nje ya nchi.
Chanzo: Mtanzania

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa