Na
Hirondelle, Arusha
Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Alhamisi amedai kwamba
Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) yenye mamlaka ya kuwashitaki
watuhumiwa wa mauaji ya kimbari,uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu,
ni fimbo ya kisiasa iliyoanzishwa kwa lengo la kuwapiga waafrika.
‘’Wanaiita mahakama ya kimataifa lakini kwa kweli ni kwa
ajili ya waafrika. Waafrika siyo lazima wale ambao wamefanya makosa, bali ni
wale wanaowapinga,’’ Rais Kagame alisema mjini Kigali wakati akizindua Mwaka wa
Mhakama wa 2012-2013 nchini humo.
Rais huyo alifafanua ’’ Wanatuambia, ooh watawaadhibu watu
wanaojihusisha katika kusajili askari watoto lakini hawawasaki wale
wanaowaua.’’
Kagame aliendelea ‘’Wapo watu wanaoua,wanaobaka na
wanaofanya kila uhalifu.Hunyamaza tu juu ya hayo yote labda ni kwa sababu tu
ndivyo waafrika wanavyotakiwa kuwa.’’
Rais huyo pia alizungumzia mgogoro unaoendelea Mashariki
mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) akidai kwamba serikali ya nchi hiyo
na jumuia ya kimataifa ndiyo inayostahili kushutumiwa na siyo Rwanda.
Baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) yameiomba
Rwanda kuunga mkono juhudi za kumtia mbaroni Jenerali Bosco Ntaganda, ambaye
anatakiwa na ICC kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.Lakini Rais
Kagame amekuwa wakati wote akidai kwamba nchi yake haina sababu yoyote ya
kufanya hivyo.
NI/FK
© Hirondelle News Agency
© Hirondelle News Agency
0 comments:
Post a Comment