Na Eliya Mbonea, Arusha
SERIKALI imeombwa kukemea vitendo vya unyanyasaji
vinavyofanywa na waajiri, dhidi ya waongoza watalii pindi ajali inapotokea
wakiwa kazini, kwani huachwa wakiteseka.
Hayo yalisemwa jana mjini hapa na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Waongoza Watalii Tanzania (TTGA), Oswald Kafana mbele ya Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Anjela Kariuki.
“Tunaiomba Serikali ikemee unyanyaswaji unaofanywa na baadhi ya waajiri wetu, hasa inapotokea ajali, sisi huwa tunaachwa tukiteseka eneo husika la ajali na waajiri wetu kukimbilia kushughulikia watalii peke yao,” alisema Kafana.
Watalii wanaokuwa wamepata ajali mara nyingi, hujikuta wakikimbizwa kupatiwa matibabu, lakini mwongozaji aliyekuwa nao huachwa akiendelea kuhangaika pekee yake, hii si haki hata kidogo,” alisema.
Alisema taasisi hiyo, ilianzishwa mwaka 1999, ambapo mpaka sasa ina wanachama 3,000, huku lengo lake kuu likiwa ni kutangaza,kuhamasisha na kulinda maslahi ya waongoza watalii, kutunza mazingira na vivutio vyote vya utalii.
Alikemea vikali tabia ya waajiri wao kusingizia uchumi duniani, unasababisha wao kushindwa kuajiriwa, badala yake wanachukua waongozaji wa muda kama kibarua, kisha kuwaachisha kazi pindi kazi za utalii zinapopungua.
Kwa upande wake, mgeni rasmi katika kikao hicho kilichokuwa kimelenga kupokea mawazo na changamoto zinazowakabili waongoza watalii hao, Naibu Waziri Kairuki alikemea vikali tabia ya baadhi ya waajiri wa waongoza watalii, kunyanyasa wafanyakazi wao.
“Unyanyasaji unaofanywa na baadhi ya waajiri, linaendana na tatizo la kutokuwapo mikataba ya ajira na suala la maslahi, hivyo tukiweza kutatua tatizo la mikataba ya ajira, mambo mengine yatafanikiwa,” alisema Kariuki.
Alisema, anavitambua vitendo vya unyanyasaji, vinavyofanywa na baadhi ya waajiri hivyo aliahidi kuvishughulikia, huku mambo mengi yaliyo juu ya uwezo wake akiahidi kuyafikisha Wizara ya Kazi na Ajira.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Ayoub Laizer alisema, umefika wakati muafaka kwa sekta hiyo, kufanywa taaluma kamili kufikiriwa na kufanywa kuwa taaluma kamili itakayowafanya watambulike kama ilivyo kwa taaluma nyingine ikiwamo Ualimu.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment