na Grace Macha, Arusha
MFUKO wa
Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF) unabadili mfumo wake
wa huduma ili uendane na ule wa kibenki ambapo utawawezesha wanachama kutumia
kadi wakati wa kudai mafao yao tofauti na sasa ambapo hutakiwa kuwa na nyaraka
mbalimbali ikiwemo barua ya ajira.
Aidha, mfuko
huo unaanzisha mfumo utakaowawezesha wanachama kupata taarifa za michango yao
kupitia simu zao za kiganjani, hivyo kuwaondolea usumbufu wa kulazimika kwenda
zipata kwenye matawi yao.
Hayo
yalibainishwa mwishoni mwa wiki mjini hapa na Mkurugenzi Mkuu wa LAPF, Eliudi
Sanga, alipozungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya mkutano wao
mkuu wa tano unaotarajia kuanza leo ambao kaulimbiu yake ni ‘Hifadhi ya jamii
na ukuaji wa uchumi’.
Alisema
maboresho hayo ni mwendelezo wa malengo ya mfuko huo katika kuhakikisha
wanachama wake wananufaika zaidi kwa kuwawezesha kumudu maisha kabla na baada
ya kustaafu.
“LAPF ni mfuko
pekee wa kijamii ambao wanachama huchangia kiasi kidogo cha asilimia 5 ya
mshahara wao huku waajiri wakichangia asilimia 15 tofauti na mifuko mingine
ambayo mwanachama huchangia asilimia 10 na mwajiri asilimia 10, tunataka
mwanachama amudu maisha, atunze familia yake vizuri, aweze kuwasomesha watoto
wake,” alisema Sanga.
Chanzo: Tanania Daima
0 comments:
Post a Comment