Naibu Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Dk. AshaRose Migiro
akiongea na waandishi wa habari
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
(TAMISEMI) Hawa Ghasia , akiongea wakati wa mkutano huo
Idd
Uwesu, Arusha Yetu
Baraza
la Viongozi Wakuu wa Serikali za Mitaa la Afrika Mashariki (EALGF) limezinduliwa
rasmi jijini Arusha huku viongozi hao wakitakiwa kulitumia baraza hilo
kikamilifu ili kutoa mchango mkubwa wa maendeleo endelevu ya wananchi wa nchi
wanachama ambao wanawahudumia
Baraza
hilo lililoundwa kutokana na maazimio ya Mkutano wa nchi wanachama uliofanyika
huko Kigali Rwanda mwaka jana limezinduliwa na Naibu Katibu Mkuu wa zamani wa
Umoja wa Mataifa Dk. AshaRose Migiro.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa Baraza hilo Dk. Migiro amesema kuwa serikali za mitaa
kama mdau wa karibu wa wananachi katika mifumo ya tawala za nchi zinalo jukumu
kubwa la kuahakikisha zinatoa huduma nzuri kwa wananchi wao hivyo uwepo wa
baraza hilo utazisaidia kuja na mikakati iliyobora zaidi katika kutekeleza
majukumu yao.
Nae
waziri mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia, amesema baraza hilo limedhamiria
kuwawezesha viongozi wenye dhamana hiyo kufanya kazi kwa pamoja katika
kuimarisha utendaji wa Serikali za Mitaa na utekelezaji wa dhana ya ugatuaji wa
madaraka kwa Umma, kwa lengo la kuleta maendeleo endelevu katika kanda ya
Afrika Mashariki.
Kupitia
mkutano huu pia viongozi hawa watapata nafasi nzuri ya kubadilishana uzoefu
kuhusu namna ya uwakilishi wa wananchi unavyofanyika, kupitia Mamlaka za
Serikali za Mitaa kama vyombo vya Uwakilishi wa wananchi katika Jumuiya ya
Afrika Mashariki, huku Nchi za Visiwa vya Comoro na Sudan ya Kusini pamoja na
wadau wengine wa maendeleo kama Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
na Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) wakialikwa
kushiriki.
Blogzamikoa




0 comments:
Post a Comment